NSSF YAJIVUNIA FAIDA TRILIONI MOJA
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesema umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake kwa kupata faida ya Sh trilioni moja.
Akizungumza Septemba 23,2023 Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema mafanikio hayo yamechangiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji hatua iliyoongeza wachangiaji katika mfuko huo.
Na Nora Damian, Geita

Mshomba alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita,
“Mfuko wa NSSF umezidi kufanya kazi vizuri na kuwa na utendaji mzuri hasa katika miaka ya karibuni hususani katika miaka ambayo mheshimiwa Rais Samia amekuwa madarakani.
“Kwa mara ya kwanza tangu mfuko uanzishwe 1964 tumeweza kupata faida ya zaidi ya shilingi trilioni moja, mfuko kwa sasa una thamani ya zaidi ya shilingi trilioni saba ambazo zimeongezeka kutoka shilingi trilioni 4.8 miaka mitatu iliyopita,” amesema Mshomba.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akimweleza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko (katikati), mafanikio ya mfuko huo baada ya kutembelea banda lao kwenye Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Kwa mujibu wa Mshomba, thamani ya michango katika mfuko huo imeongezeka kutoka Sh trilioni 1.48 mwaka 2022 hadi kufikia Sh trilioni 1.66 mwaka 2023.
Amesema pia wamefaidika kwa kuongeza wanachama mkoani Geita hatua iliyosaidia kuongeza makusanyo kutoka Sh bilioni 29 hadi zaidi ya Sh bilioni 56 mwaka 2022.
Mkurugenzi huyo amesema wamepata mafanikio kwa kushiriki Maonyesho ya Teknolojia ya Madini tangu yalipoanzishwa mwaka 2018 na kuwataka wananchi wa Geita kutumia fursa ya maonyesho hayo kujiunga na mfuko.
“Maonyesho haya kwetu ni muhimu sana kwa sababu yanatuwezesha kusajili wanachama wa mfuko walioko katika sekta binafsi na isiyo rasmi na kuwawezesha kuondokana na umaskini hata baada ya kukosa uwezo wa kufanya kazi mfano wanapofikia uzee au wanapougua,” amesema Mshomba.
Amesema wanatarajia ofisi na majengo ya uwekezaji mkoani Geita ili kuongeza wigo wa utoaji huduma na kuwataka wananchi kuzingatia hifadhi ya jamii kwani itawawezesha kupambana na umaskini.