WAKANDARASI MRADI WA MAJI SAME - MWANGA - KOROGWE WATAKIWA KUONGEZA KASI


Na Mwandishi Wetu, Moshi

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Jamal Katundu amewataka wakandarasi wanaojenga mradi wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe kukamilisha kazi hiyo haraka ili wananchi wanufaike kwa kupata huduma ya maji.

Profesa Katundu ameyasema hayo baada ya kukagua mradi huo na kusema ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wake.

Mradi huo unatarajiwa kutatua changamoto ya muda mrefu za upatikanaji wa maji kwa wananchi.


Amesisitiza umuhimu wa kuzingatia ratiba ya utekelezaji wa mradi na ikiwezekana kazi ifanyike na kukamilika kabla ya muda uliopangwa kwa sababu huduma ya maji ni haki ya msingi na Serikali imejipanga kufanikisha jambo hilo kwa wananchi.

Kiongozi wa Timu ya Uratibu wa Mradi Mhandisi Abbas Pyarali, amesema hadi Agosti 31, 2023 utekelezaji wa mradi huo ulikuwa umefika asilimia 79.5.
Powered by Blogger.