MIPAKA YAIMARISHWA HIFADHI YA MAKUTOPORA



Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Maelekezo ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kuhusu kuhifadhi na kuendeleza vyanzo vya maji yameanza kutekelezwa katika eneo la Hifadhi ya Makutopora jijini Dodoma.

Waziri Aweso alitoa maelekezo hayo hivi karibuni katika kikao kazi na watendaji wa sekta ya maji ambapo alisisitiza ili huduma ya maji iwe endelevu ni muhimu kwa kila kiongozi na wananchi kushirikishwa katika kazi ya uhifadhi.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabbir Shekimweri, ametembelea eneo la hifadhi ya maji chini ya ardhi - Makutopora na kukagua utekelezaji wa maagizo ya shughuli za uhifadhi wa eneo hilo zinazoendelea.


 Shekimweri amekagua njia zilizochongwa kwa ajili ya kuzuia adhari za moto zenye urefu wa kilomita 22, alama za mipaka kuonyesha mwanzo wa hifadhi na mwisho wa hifadhi pamoja na kukagua alama za kudumu za mipaka.

Mkuu huyo wa wilaya ameridhishwa na utendaji kazi uliofanyika ikiwamo ujenzi wa alama za kudumu zenye ukubwa wa mita mbili jambo litakalosaidia kupunguza uvamizi kwa visingizio vya kutokufahamu eneo la hifadhi.


 Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Dodoma imetoa pongezi kwa ubunifu wa njia zilizochongwa kwa sababu zimekidhi viwango vya uzuiaji wa moto hivyo kero za moto kushambulia eneo kubwa zitapungua.
Powered by Blogger.