MRADI WA MAJI SAME ASILIMIA 80
Na Mwandishi Wetu, Same
Utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Same - Mwanga - Korogwe umefikia asilimia 80.
Kiongozi wa Timu ya Uratibu wa mradi huo, Mhandisi Abbas Pyarali, amesema hivi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 80 na kazi zinazoendelea kwa kasi ni pamoja na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme, miundombinu ya kusafirisha malighafi, eneo la kutibu maji na miundombinu ya kusafirisha maji kwenda eneo la Kisangara.
Mradi huo unatekelezwa mkoani Kilimanjaro kwa kutumia chanzo cha maji cha Nyumba ya Mungu na wakandarasi wanaohusika kwa kazi mbalimbali ni Kampuni za Ms MA Kharafi & Sons, Ms Advent, Ms Help Desk na Central Electrical.
Uongozi wa Wizara ya Maji umewataka wakandarasi hao kufanya kazi saa 24 ili wananchi waanze kupata huduma ya maji kupitia mradi huu na 'kumtua mama ndoo ya maji kichwani'.



