WACHIMBAJI MERERANI WAMWANGUKIA RAIS SAMIA GHARAMA ZA UMEME
Katibu wa Chama cha Wachimbaji Mkoa wa Manyara, Rachel Njau (kushoto), akiwa kwenye Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika eneo la Mererani mkoani Manyara wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati gharama za umeme wanazotozwa ambazo wamedai kuwa ni kubwa.
Akizungumza Septemba 22,2023 wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini lililofanyika katika Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, Katibu wa Chama cha Wachimbaji Mkoa wa Manyara, Rachel Njau, amesema baadhi yao tayari wamepewa notisi na kampuni ya udalali iliyopewa jukumu la kudai madeni hayo.
Wachimbaji hao wanaodaiwa na Shirika la Umeme (Tanesco) wamepewa notisi ya siku 14 na kampuni hiyo kulipa madeni husika vinginevyo mali zao zitapigwa mnada.
Njau amedai kuwa mita walizofungiwa zimekuwa zikisoma hata kama hawafanyi kazi au umeme ukikatika.
“Umeme ukiwepo, tusipofanya kazi zile mita walizoziweka zina – operate kwahiyo bili inakuja, mtu mmoja anaweza akaletewa bili ya shilingi milioni 18 mpaka 20 kwa mwezi.
“Zile mita hazikuwepo zamani, kulikuwa na mita za luku zilizokuwa zinatumika, tunaomba turejeshewe mita za luku ambazo zina – operate kuanzia uniti 70,000 kwa mwezi,” amesema Njau.
wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini lililofanyika katika Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.
Amesema luku hizo zina uwezo wa kuhimili matumizi ya mgodini kuliko wanazotumia sasa za ‘P2 Panel Power’ ambazo zilifungwa baada ya kuondolewa luku.
“Uchimbaji wa madini ya Tanzanite ni tofauti na mengine, tunachukua muda mrefu kupata, ufanye kazi au usifanye kazi lazima utakuta bili inakuhusu kwahiyo ni changamoto kubwa kwetu na umeme Mererani unakatika mara kwa mara.
“Nimuombe mama yetu Rais Samia atusaidie wachimbaji wadogo waangalie jinsi ya kutatua tatizo hili vinginevyo watatufilisi. Sisi tunapenda kulipa kodi hatutaki kulimbikiza madeni tunaomba watuwekee luku zinazostahili,” amesema Njau.
The page imefanikiwa kuona baadhi ya notisi zilizotumwa kwa wachimbaji hao ambapo baadhi yao wanadaiwa Sh 50,267,631.22 huku wengine wakidaiwa Sh 14,547,025.93.
Akijibu madai hayo Mwakilishi wa Tanesco ambaye pia ni Meneja wa Mkoa wa Geita, Grace Ntungi, amesema shirika hilo linawadai wachimbaji sehemu mbalimbali nchini na kutolea mfano Geita ambapo wanawadai zaidi ya Sh bilioni moja.
“Wajibu wa kulipa ankara ni wetu, kama zitakuwa hazilipwi huduma zitakwendaje?
“Geita tunadai zaidi ya shilingi bilioni moja…fikeni ofisini tujadiliane namna ya kulipa,” amesema Ntungi.