FCC YAELEZA MIKAKATI KUDHIBITI BIDHAA BANDIA
Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, akizungumza wakati wa mafunzo kwa wachimbaji madini wanaoshiriki Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Tume ya Ushindani (FCC) imesema imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kudhibiti uagizaji, uingizaji na utumiaji wa bidhaa bandia.
Hivi karibuni tume hiyo ilifungua ofisi za kanda tatu ambazo ni Kanda ya Ziwa, Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kuongeza wigo wa kuwafikia Watanzania na kuwapa elimu juu ya athari za bidhaa bandia na kumlinda mlaji.
Hayo yamesemwa leo Septemba 22,2023 na Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, wakati wa mafunzo kwa wachimbaji madini wanaoshiriki Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita.
“Tunaendelea na mapambano ya bidhaa bandia, tunaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kama si kupunguza basi tunatokomeza kabisa bidhaa bandia.
“Tunatoa elimu kwa wadau mbalimbali kupitia semina, makongamano, mikutano na maonyesho kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 na Sheria ya Alama za Bidhaa ya mwaka 1963.
“Walaji wanatakiwa kufahamu kuwa watengenezaji wa bidhaa bandia huwa wanazalisha bidhaa rahisi ambazo zinakubalika zaidi sokoni, hivyo ni vizuri tukashirikiana na wadau wote kuhakikisha tunazitokomeza,” amesema Nsajigwa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, akizungumza wakati wa siku ya watoa huduma na leseni za uchimbaji madini na uwezeshaji mitaji kwa washiriki wa Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Amesema tume hiyo ina jukumu la kulinda ushindani kwa lengo la kumlinda mlaji na mtumiaji na kukuza uchumi wa soko.
Kwa mujibu wa Nsajigwa katika jitihada za kudhibiti bidhaa bandia, wiki iliyopita tume hiyo iliteketeza bidhaa zilizokamatwa mwaka 2022 zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 900.
Amesema pia walifanya kaguzi katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu ambapo asilimia 3.4 ya makasha yenye thamani ya Sh bilioni 20.8 yalikuwa na bidhaa zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa.
Aidha amesema kaguzi za kushtukiza zilifanyika ambapo bidhaa zenye thamani ya Sh bilioni 4.7 zilizokiuka Sheria ya Alama za Bidhaa zilikamatwa na hatua kuchukuliwa.
Ofisa huyo amesema kaguzi hizo zilifanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Songwe, Kilimanjaro, Pwani, Arusha, Mwanza, Katavi na Geita.
Akifunga mafunzo hayo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, amesisitiza taasisi za serikali na wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana ili kumlinda mlaji na kudhibiti matumizi ya bidhaa bandia.
“Tunataka kuona maendeleo tunayoenda nayo kwa kasi yawe endelevu na madhara yawe kidogo,” amesema Kigahe.