VYETI 400 VYA KUZALIWA VYATOLEWA MAONESHO YA MADINI GEITA
Wakili wa Serikali kutoka RITA, Salvius Rwechungura, akimweleza Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (Kulia), shughuli zinazofanywa na wakala huo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) umetoa vyeti vya kuzaliwa zaidi ya 400 kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kupitia Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini.
Rita imeshiriki katika maonesho hayo yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili, mkoani Geita kwa kutoa elimu ya masuala mbalimbali pamoja na huduma za utoaji vyeti vya kuzaliwa.
Akizungumza Septemba 29,2023 Wakili wa Serikali kutoa Rita, Salvius Rwechungura, amesema shughuli za utoaji vyeti vya kuzaliwa zinafanyika kielektroniki na ndani ya saa moja muhusika anapata cheti.
Rwechungura alikuwa akizungumza baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kutembelea banda la wakala huo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika.
Amesema pia mbali ya kutoa vyeti wanatoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya ndoa na talaka na umuhimu wa kuandika wosia.
“Kuna watu wanagombania urithi, wananyimwa urithi, watoto wanashindwa kunufaika na mali za wazazi wao kwa sababu mzazi hakuandika wosia.
“Kuandika wosia sio kujitabiria kifo, ni namba ya kuweka utaratibu wa usimamizi wa mali hata nyakati ambazo hatupo. Badala ya jamii kutumia muda mwingi wanagombania mirathi watumie muda huo kuzalisha,” amesema Rwechungura.
Amesema katika maonyesho hayo changamoto kubwa ambayo wamebaini ni uelewa mdogo katika kuhifadhi wosia.
“Wengi wana fikra kwamba wakiandika wosia wataondoka kesho, kumbe si sahihi, tunajaribu kuwaelimisha. Mtu anapotafuta mali kwa jasho halafu inatokea zikashindwa kuwanufaisha wahusika wake haileti picha nzuri kwenye familia.
“Kwahiyo tunawasisitiza kuandika na kumshirikisha mwenza mali walizonazo na mahali zilipo kwa sababu kuna nyakati tunateuliwa na mahakama kusimamia mirathi.
“Ukisimamia mirathi ambayo mali zake zinafahamika zipo sehemu fulani inakuwa rahisi, lakini ukipata mirathi ambayo hata mwenye mali hakuacha taarifa inabidi ufanye jitihada za kujua hizo mali ambazo mwenye nazo hakuiambia familia,” amesema.
Mmoja wa wakazi wa Geita aliyepatiwa cheti cha kuzaliwa Manasseh Elias, amesema; “Naipongeza Rita kwa kuamua kuja kutuletea huduma hii kwenye maonesho haya, nimekuja leo wamenihudumia na nimepata cheti changu cha kuzaliwa.
Waziri Mavunde ameupongeza wakala huo na kushauri uendelee kusogeza huduma kwa kuwa bado wananchi wengi wana uhitaji.
Na Nora Damian, Geita