SGA YATEKELEZA SHERIA UWEZESHAJI WAZAWA KWA KUAJIRI VIJANA 1,200
Ofisa Masoko wa Kampuni ya SGA, Flora Fanuel, akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita.
Vijana 1,200 wamepata ajira katika Kampuni ya Ulinzi ya SGA ambayo ina zabuni za kulinda maeneo mbalimbali nchini ikiwemo migodi.
Sheria ya Uwezeshaji Wazawa (Local Content) ya mwaka 2018 inahimiza kutolewa fursa kwa Watanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini.
Akizungumza Septemba 29,2023 Ofisa Masoko wa SGA, Flora Fanuel, amesema wanatoa huduma za ulinzi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki kama vile CCTV kamera na mingine.
Flora alikuwa akizungumza baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kutembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya SGA, Flora Fanuel, akionesha mfumo wa uzio wa umeme katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Vijana 1,200 wamepata ajira katika Kampuni ya Ulinzi ya SGA ambayo ina zabuni za kulinda maeneo mbalimbali nchini ikiwemo migodi.
Sheria ya Uwezeshaji Wazawa (Local Content) ya mwaka 2018 inahimiza kutolewa fursa kwa Watanzania ili waweze kushiriki kikamilifu katika uchumi wa madini.
Akizungumza Septemba 29,2023 Ofisa Masoko wa SGA, Flora Fanuel, amesema wanatoa huduma za ulinzi kwa kutumia mifumo ya kielektroniki kama vile CCTV kamera na mingine.
Flora alikuwa akizungumza baada ya Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, kutembelea banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita.
Amesema katika Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) wameajiri wafanyakazi zaidi ya 700 na kwamba hivi sasa wana mkataba mpya katia Mgodi wa Barick ambapo wameajiri vijana zaidi ya 500.
“Tunatekeleza Sheria la Local Content kwa asilimia 100, tunaamini dhahabu ni kitu ambacho kinahitajika sana hivyo tumekuja na suluhisho.

"Tunakulinda unafanya uzalishaji ukimaliza tunakusafirishia sdhahabu yako kwa kutumia magari yetu yanayotumika kusafirisha fedha.
“Tutachukua mzigo wako kama utataka tuupeleke maabara kwa ajili ya uchenjuaji au kwa mteja utafika salama…gharama zetu ni ndogo na zimetofautiana, gharama tutakayompa mchimbaji mkubwa ni tofauti na tutakayompa mchimbaji mdogo ili wote tuweze kuwahudumia,” amesema Flora.
Ameshauri wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutumia kampuni za ulinzi kwa sababu wanaweza kutumia nguvu kubwa kufanya uzalishaji halafu mizigo ikaibiwa.
Waziri Mavunde ameipongeza kampuni hiyo na kuwataka wawekezaji katika sekta ya madini kuitumia ili kuongeza ufanisi katika shughuli zao.