MAVUNDE APONGEZA UBUNIFU WA TANRADE KLINIKI YA BIASHARA
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (Kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Biashara wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Msimamizi wa Kliniki ya Biashara katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini, Samirah Mohamed (kulia), kuhusu kliniki iliyopo kwenye maonesho hayo viwanja vya EPZ Bombambili mkoani Geita.
Kliniki ya biashara iliyopo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini imewezesha utatuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya biashara kwa kuzitafutia suluhisho.
Kliniki hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na taasisi za umma zinazoshughulikia masuala ya biashara katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya taasisi za umma zilizopo katika kliniki hiyo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGLA), Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Tume ya Ushindani (FCC).
Watembeleaji wa maonesho hayo yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita wakiwemo viongozi mbalimbali wamekuwa wakifika na kupata elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizo.
Septemba 29,2023 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ametembelea kliniki hiyo na kuipongeza TanTrade kwa ubunifu huo.
“Haya ni maendeleo makubwa, naamini taasisi zilizopo katika kliniki hii zimejenga uelewa kwa wananchi wetu na washiriki wa maonesho kuhusu masuala mbalimbali yaliyopo katika sekta ya madini…nawapongeza sana,” amesema Mavunde.
Mwonekano wa Kliniki ya Biashara inayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) iliyopo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
“Katika maonesho mbalimbali ambayo Tantrade inaratibu kama ya kimataifa, kisekta na ya kanda tunakuwa na kiliniki ya biashara. Lengo ni kuzikutanisha taasisi na wale wanaowahudumia na kuwapatia elimu ya shughuli zao lakini pia kutatua changamoto na malalamiko waliyonayo,” amesema Samira.
Amesema pia mamlaka hiyo inaratibu ushiriki wa Tanzania kwenye maonesho ya dunia, misafara ya kibiashara na mikutano ya wafanyabiashara.
Ofisa Mkaguzi na Mfuatiliaji wa Bidhaa Bandia wa FCC Kanda ya Ziwa, Mgasi Kalindimya, amesema kupitia kliniki hiyo wanatoa usaidizi wa kitaalamu na ushauri wa masuala mbalimbali yanayohusu tume hiyo.
Na Nora Damian, Geita
Kliniki ya biashara iliyopo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini imewezesha utatuzi wa changamoto zinazoikabili sekta ya biashara kwa kuzitafutia suluhisho.
Kliniki hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kushirikiana na taasisi za umma zinazoshughulikia masuala ya biashara katika sekta mbalimbali.
Baadhi ya taasisi za umma zilizopo katika kliniki hiyo ni Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (CGLA), Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Tume ya Ushindani (FCC).
Watembeleaji wa maonesho hayo yanayofanyika viwanja vya EPZA, Bombambili mkoani Geita wakiwemo viongozi mbalimbali wamekuwa wakifika na kupata elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hizo.
Septemba 29,2023 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ametembelea kliniki hiyo na kuipongeza TanTrade kwa ubunifu huo.
“Haya ni maendeleo makubwa, naamini taasisi zilizopo katika kliniki hii zimejenga uelewa kwa wananchi wetu na washiriki wa maonesho kuhusu masuala mbalimbali yaliyopo katika sekta ya madini…nawapongeza sana,” amesema Mavunde.
Ofisa Biashara Tantrade na Msimamizi wa kliniki hiyo, Samira Mohamed, amesema kliniki ya biashara imewezesha utatuzi wa changamoto na matatizo yanayoikabili sekta ya biashara na kuyatafutia suluhisho.