TAWOMA KUADHIMISHA MIAKA 25 KWA KUMPATA MALKIA WA MADINI
Mwenyekiti wa Tawoma Taifa, Semeni Malale.
Chama cha Wachimbaji Wanawake Tanzania (TAWOMA) kimesema kitamtangaza mchimbaji anayeongoza kwa ulipaji kodi na tozo mbalimbali za Serikali ili kuongeza Pato la Taifa kupitia tasnia ya uchimbaji wa madini.
Chama hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1997 hadi sasa kina wanachama 4,000 katika mikoa 21.
Akizungumza Septemba 21,2023 na waandishi wa habari kwenye Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Madini katika viwanja vya EPZA mkoani Geita, Mwenyekiti wa TAWOMA Taifa, Semeni Malale, amesema mchakato huo ulianza kwa kupita migodini kwa lengo la kuhamasisha ulipaji kodi na tozo za Serikali.
“Malkia wa madini tunaangalia nani anayeongoza kwa ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali za Serikali, huduma za usalama migodini, afya na mazingira, anayesaidia jamii na kutoa ajira.
“Tutakapompata malkia wa madini tunaamini na kinamama wengine watahamasika kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali na kuzingatia usalama katika shughuli zao.
“Sisi tunachokitaka ni kuongeza Pato la Taifa kupitia tasnia ya uchimbaji wa madini, mpaka sasa tunajivunia miaka 25 ya Tawoma kinamama tunajiamini, tunafanya kazi na tunalipa tozo na stahiki zote za Serikali,” amesema Malale.
Zahanati ya Kijiji cha Nyamishiga iliyojengwa na wanawake wachimbaji madini.
Amesema wanao vijana wanaojiunga na chama hicho wakitokea vyuo vikuu (TAWOMA YOUTH) ambao wamekuwa wakijiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za uongezaji thamani madini.
Hata hivyo amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya mitaji kwa sababu taasisi nyingi za fedha haziwaamini wachimbaji na kuiomba Serikali kutoa ruzuku kwa wanawake wachimbaji.
“Bado tunahitaji maeneo ya kuchimba, mama Samia alisema kuna mapori tengefu watu waachiwe kuchimba, tunaomba watakapoyaachia tumilikishwe kinamama kwa sababu sisi ni waaminifu, tunachimba vizuri na tunalipa tozo na mirabaha ya Serikali na kusaidia jamii inayotuzunguka,” amesema Malale.
Na Nora Damian, Geita

Aidha amesema wanajivunia uwepo wa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na jitihada alizozifanya za kufungua mipaka ya nchi hatua iliyowezesha kuongezeka kwa fursa katika sekta ya madini.
“Katika uongozi wa mama Samia wanachama wengi wamenufaika kwa sababu baada ya mama mwenzetu kuchukua madaraka tuliheshimika. Kwenye migodi tulianza kufanya kazi na kupata masilahi, masoko yapo kutokana na mama kufungua nchi hivyo wawekezaji ni wengi,” amesema.
Malale ambaye pia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Mshikamano cha wanawake wachimbaji madini Kahama amesema wamekuwa wakirudisha sehemu ya faida wanayoipata kwenye jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu.
Amesema wamejenga zahanati katika Kijiji cha Nyamishige iliyopo Halmashauri ya Msalala Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga iliyogharimu Sh milioni 230, kununua gari la kubebea wagonjwa lenye thamani ya Sh milioni 75 na madawati 100.

Gari la wagonjwa lililonunuliwa na wanawake wachimbaji madini.