STAMICO KUNUNUA MITAMBO 15 YA WACHIMBAJI WADOGO
Mjiolojia Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), Alex Rutagwelela, akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini wanaoshiriki Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Shirika la Madini la Taifa (Stamico) limesema limeagiza mitambo 15 kwa ajili ya kuendeleza shughuli za wachimbaji wadogo.
Akizungumza Septemba 25,2023 wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini wanaoshiriki Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini mkoani Geita, Mjiolojia Mkuu, Alex Rutagwelela, amesema shirika hilo kwa sasa lina mitambo 31.
“Tumefanya ‘study’ kubwa kupitia wachimbaji wadogo, Serikali imesikia kilio kwamba mitambo inayokuja ni midogo.
“Tumeandaa andiko ambalo litakuwa linaeleza Stamico itafanya nini na mchimbaji mdogo atafanya nini, kabla ya kufika kwa mchimbaji mdogo tutampatia wasilisho hilo,” amesema Rutagwelela.
Amesema gharama kubwa zitabebwa na Stamico tofauti na uchorongaji wa kawaida wa kibiashara na kwamba mitambo hiyo ina uwezo wa kuchimba mita 150 chini ya ardhi kwa gharama nafuu.
Aidha amesema katika migodi yote iliyopo nchini Stamico imefanya uchorongaji na kwamba wana mifumo miwili ya uchorongaji yaani wa kutumia upepo na maji.
Mjiolojia huyo amesema wamekuwa wakifanya uchorongaji wa miamba, uchakataji wa miamba, kuuza kemikali za uchenjuaji, ununuzi wa dhahabu na kuwaunganisha wachimbaji wadogo na taasisi za fedha pamoja na makampuni yanayojihusisha na uuzaji vifaa kazi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Dk. Venance Mwasse, akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi za Kampuni ya GF Trucks and Equipment Geita, amesema wanasogeza huduma sehemu za wachimbaji ili kuongeza ufanisi.
Amesema miongoni mwa mambo waliyokubaliana na kampuni hiyo ni kusogeza huduma sehemu za wachimbaji na kuwauzia au kuwakodishia vifaa.
“Tukio la leo ni utekelezaji wa miongoni mwa mambo ambayo tulikubaliana, jambo lingine tulilokubaliana ni kukodisha vifaa pamoja na kuuza.
“Sekta ya madini inahitaji mtaji mkubwa au uwekezaji mkubwa, lakini inahitaji muda mrefu. Ukimuangalia mchimbaji mdogo si lazima awe na resource (rasilimali) nyingi, anaweza akachimba bila kuwa na uwekezaji wa muda mrefu.
“Kwahiyo tukaona tukae pamoja tujadiliane tuone namna ya kumrahisishia mchimbaji mdogo asipate presha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kumiliki trucks, bludoza ndio aweze kuchimba,” amesema Dk. Mwasse.