MAVUNDE AIPONGEZA GF TRUCKS KUFUNGUA OFISI GEITA, KUUNGANISHA MAGARI 1,500
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi za Kampuni ya GF Trucks & Equipment mkoani Geita. Kulia ni Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu.
Na Nora Damian, Geita
Kampuni ya GF Trucks and Equipment imefungua ofisi mkoani Geita huku ikipanga kuunganisha magari 1,500 mwaka huu.
Akizungumza leo Septemba 25,2025 wakati wa uzinduzi wa ofisi hizo zilizopo katika Soko Kuu la Dhahabu Geita,
Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kampuni hiyo, Salman Karmali, amesema hatua hiyo inatokana na makubaliano waliyoingia na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
Amesema Stamico lina vifaa vya kuchoronga na kufanya tafiti huku kampuni hiyo ikitoa mashine na maroli.
“Geita inategemea uchimbaji kwa asilimia kubwa na sisi tunategemea wana Geita, magari tunayouza ni matunda mazuri ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji," amesema Karmali.
Mkurugenzi wa Masoko na Biashara wa Kampuni ya GF Trucks & Equipment, Salkmani Karmali, akimkabidhi tuzo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, baada ya kufungua ofisi za kampuni hiyo mkoani Geita.
Amesema pia wamefanya upanuzi wa kiwanda kwa lengo la kuanza kuunganisha magari madogo na mwaka huu wanatarajia kuunganisha magari 1,500.
Mkurugenzi huyo amesema wamekubaliana kuweka mashine karibu na wachimbaji ili kuwa karibu na wachimbaji wadogo.
Mkurugenzi Mkuu wa Stamico, Dk. Venance Mwasse, amesema walikubaliana kusogeza huduma sehemu za wachimbaji na kuwauzia au kuwakodishia vifaa.

“Sekta ya madini inahitaji mtaji mkubwa au uwekezaji mkubwa, lakini inahitaji muda mrefu.
"Ukimuangalia mchimbaji mdogo si lazima awe na resource (rasilimali) nyingi, anaweza akachimba bila kuwa na uwekezaji wa muda mrefu. Tulijadiliana na kuona namna ya kumrahisishia mchimbaji mdogo asipate presha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kumiliki trucks au bludoza ndio aweze kuchimba,” amesema Dk. Mwasse.
Meneja wa Benki ya CRDB Geita, Efrosina Mwanja, amesema wanashirikiana na kampuni hiyo kuwakopesha wachimbaji magari na vifaa.
Kwa mujibu wa Meneja huyo kupitia makubaliano hayo mchimbaji anayehitaji gari au vifaa kazi huchangia asilimia 30 ya gharama kisha asilimia 70 hukopeshwa na benki hiyo.
“Tunawakopesha wafanyabiashara au wachimbaji, atachangia asilimia 30 ya gharama yote ya manunuzi ya gari au vifaa. Kwahiyo tunatoa asilimia 70 ya gharama na dhamana ni kile chombo ulichonunua,” amesema Mwanja.
Benki hiyo pia imekuwa ikiwapeleka wachimbaji wadogo nje kama vile China, Dubai na Uturuki kwa lengo la kujifunza na kupata ufanisi katika shughuli za madini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale, Grace Kingalame, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofisi za
"Ukimuangalia mchimbaji mdogo si lazima awe na resource (rasilimali) nyingi, anaweza akachimba bila kuwa na uwekezaji wa muda mrefu. Tulijadiliana na kuona namna ya kumrahisishia mchimbaji mdogo asipate presha ya kuwa na mtaji mkubwa wa kumiliki trucks au bludoza ndio aweze kuchimba,” amesema Dk. Mwasse.
Meneja wa Benki ya CRDB Geita, Efrosina Mwanja, amesema wanashirikiana na kampuni hiyo kuwakopesha wachimbaji magari na vifaa.
Kwa mujibu wa Meneja huyo kupitia makubaliano hayo mchimbaji anayehitaji gari au vifaa kazi huchangia asilimia 30 ya gharama kisha asilimia 70 hukopeshwa na benki hiyo.
“Tunawakopesha wafanyabiashara au wachimbaji, atachangia asilimia 30 ya gharama yote ya manunuzi ya gari au vifaa. Kwahiyo tunatoa asilimia 70 ya gharama na dhamana ni kile chombo ulichonunua,” amesema Mwanja.
Benki hiyo pia imekuwa ikiwapeleka wachimbaji wadogo nje kama vile China, Dubai na Uturuki kwa lengo la kujifunza na kupata ufanisi katika shughuli za madini.
Kampuni ya GF Trucks & Equipment mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, ambaye alikuwa mgeni rasmi ameipongeza kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na sekta ya madini hasa wachimbaji kwa kuwapatia vifaa.
“Nawapongeza GF Trucks kwa kusogeza huduma karibu na wachimbaji, niwaombe muendelee kutanua wigo, wachimbaji ni waaminifu wanao uwezo mkubwa wa kuchukua mitambo kwa njia ya mkopo na kuirejesha,” amesema Mavunde.
Amesema pia mwaka huu Mkoa wa Geita umewekewa lengo la kukusanya maduhuli ya Serikali Sh bilioni 243 na ndiyo mkoa unaoongoza kwa mchango mkubwa wa maduhuli.
Katika hafla hiyo kampuni hiyo pia ilikabidhi maroli matatu yaliyonunuliwa na wachimbaji na kutoa tuzo kwa wadau mbalimbali akiwemo Waziri Mavunde na Mkuu wa Mkoa wa Geita kutambua mchango wao katika kuendeleza shughuli za kampuni hiyo.