NIC YANADI BIMA NNE MUHIMU KWA WACHIMBAJI
Meneja wa NIC Kanda ya Ziwa, Stella Marwa, akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini lililoshirikisha washiriki wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, mkoani Geita.
Katika jitihada za kuongeza ufanisi katika sekta ya madini Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeanzisha bima nne ikiwemo inayowafidia wachimbaji kutokana na hasara.
Kuna bima ya ajali, bima ya maisha, 'machinery breakdown' inayowafidia wachimbaji baada ya kupata hasara na bima inayotolewa kwa wamiliki wa migodi wanapofikia ukomo wa kuchimba madini na kurudisha eneo husika katika matumizi mengine ya kijamii.
Akizungumza Septemba 25,2023 Meneja wa NIC Kanda ya Ziwa, Stella Marwa, amesema bima hizo zinawawezesha wachimbaji kufanya uwekezaji unaoweza kuzisaidia familia zao pale wanapopata majanga yasiyozuilika.
Marwa alikuwa akizungumza wakati wa kongamano la wadau wa sekta ya madini lililoshirikisha washiriki wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA, mkoani Geita.
“Bima ya ajali inakulinda ukiwa ndani ya kazi na nje ya kazi, unaweza ukapata ajali mfano umefunikwa na kifusi, umejeruhiwa kwahiyo bima itakusaidia gharama zote za matibabu ambazo utatumia kujitibu kama utakuwa umepata majeraha…ukifariki warithi wako watafidiwa.
“Ukikata bima ya ‘machinery breakdown’ faida mojawapo ni kukuhakikishia kwamba hasara zote utakazokuwa umepata wakati umesimama NIC watakufidia” amesema Marwa.
Amewashauri wachimbaji kuweka akiba kwenye bima za maisha ili waweze kufanya uwekezaji unaoweza kuzisaidia familia zao pale wanapopata majanga yasiyozuilika.
“Furaha ya maisha yako ya kesho yanajengwa na maamuzi yako ya sasa, bima hii ina uwekezaji ndani yake na kinga kwenye maisha.
“Tumeshiriki Maonyesho ya Teknolojia ya Madini ili kuwaletea elimu wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa. Tunawapa elimu ya bima kuhusiana na mitambo wanayotumia katika shughuli zao za uchimbaji.
“Elimu inawasaidia mashine ikipata hitilafu asipate hasara na NIC tuweze kuitengeneza kwa haraka, tunaweza kumfidia hasara zote atakazopata wakati amesimama shughuli zake za uchimbaji,” amesema.
Kwa wamiliki wa migodi shirika hilo linatoa bima kwa kuihakikishia Serikali ikifika ukomo wa uchimbaji wa madini eneo husika litarudishwa katika hali yake ya kawaida kwa ajili ya matumizi mengine ya kijamii.
“Hakuna kemikali yoyote itakayomuathiri mtu anayezunguka maeneo ambayo uchimbaji umefika mwisho, na endapo mmiliki atashindwa kuyarudisha mazingira katika hali yake bima ya ‘rehabilitation bond’ itafanya kazi hiyo,” amesema Marwa.
Amewashauri wachimbaji kuchangamkia fursa za bima hizo ili kuongeza ufanisi kwenye shughuli zao.
Na Nora Damian, Geita

Amesema wanayo pia bima ya maisha na kwamba wanaoikata pindi wakifiwa na watu wao wa karibu kama mtoto au mwenza hufidiwa gharama za mazishi.