FCC WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI KIGAHE, KUWAFIKIA WACHIMBAJI WOTE
Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, akitoa elimu katika banda la Kampuni ya Uchimbaji Madini ya FEMA inayoshiriki Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini viwanja vya EPZA mkoani Geita.
Tume ya Ushindani (FCC) imesema itawafikia wachimbaji wote nchini na kuwaelimisha kuhusu sheria na majukumu mbalimbali wanayotekeleza ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa na mazingira bora na salama ya ufanyaji biashara nchini.
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, aliziagiza taasisi za serikali kutoa elimu kwa umma hasa wachimbaji ili wajue taratibu, kanuni na sheria waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Leo Septemba 24,2023 Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, ametembelea baadhi ya mabanda na kuwaelimisha washiriki wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita kuhusu majukumu mbalimbali yanayofanywa na tume hiyo.
“Tunatoa elimu ya masuala ya ushindani, sheria na mengine yanayohusu tume, tunapita banda kwa banda na tutakwenda pia baadhi ya migodi.
“Tutakwenda Kata ya Nyakagwe, Mtakuja, Katoro lengo ni kuhakikisha tunatumia fursa ya maonyesho haya kumfikia kila mchimbaji ili wajue matumizi sahihi ya teknolojia lazima upate elimu sahihi,” amesema Nsajigwa.
Ofisa Mkaguzi na Mfuatiliaji wa Bidhaa Bandia Kanda ya Ziwa, Mgasi Kalindimya, akionyesha bidhaa halisi (kulia) ambayo ina nembo ya TBS. Aliyoishika kushoto ni bidhaa bandia.
Amesema pia bidhaa bandia si salama kwani nyingi zinatengenezwa katika mazingira mabovu na kuwataka wananchi wafike kwenye maonyesho hayo kupata elimu waweze kuzitambua.
Amezitaja adhabu kwa mtu atakayebainika kutengeneza bidhaa bandia kuwa ni kifungo cha miaka minne hadi 15, faini ya Sh milioni 10 hadi Sh milioni 50 au thamani ya mzigo husika ambao pia huteketezwa.
“Fikiria kwamba umetoka kuchukua mkopo halafu unakamatwa na bidhaa bandia zinateketezwa, tunatoa rai wa Watanzania na wana – Geita wasijihusishe na bidhaa bandia…njooni tujifunze mbinu bora za kiushindani na mbinu za kukagua bidhaa bandia,” amesema.
Na Nora Damian, Geita
Tume ya Ushindani (FCC) imesema itawafikia wachimbaji wote nchini na kuwaelimisha kuhusu sheria na majukumu mbalimbali wanayotekeleza ili kutimiza azma ya Serikali ya kuwa na mazingira bora na salama ya ufanyaji biashara nchini.
Hivi karibuni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, aliziagiza taasisi za serikali kutoa elimu kwa umma hasa wachimbaji ili wajue taratibu, kanuni na sheria waweze kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Leo Septemba 24,2023 Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, ametembelea baadhi ya mabanda na kuwaelimisha washiriki wa Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita kuhusu majukumu mbalimbali yanayofanywa na tume hiyo.
“Tunatoa elimu ya masuala ya ushindani, sheria na mengine yanayohusu tume, tunapita banda kwa banda na tutakwenda pia baadhi ya migodi.
“Tutakwenda Kata ya Nyakagwe, Mtakuja, Katoro lengo ni kuhakikisha tunatumia fursa ya maonyesho haya kumfikia kila mchimbaji ili wajue matumizi sahihi ya teknolojia lazima upate elimu sahihi,” amesema Nsajigwa.
Kampuni ya Uchimbaji Madini ya FEMA ni miongoni mwa waliopatiwa elimu ambapo Msimamizi wa Miradi wa kampuni hiyo, Razack Kimaro, ameishukuru tume hiyo na kuishauri iendelee kutoa elimu kwa wachimbaji.
Naye Ofisa Mkaguzi na Mfuatiliaji wa Bidhaa Bandia Kanda ya Ziwa, Mgasi Kalindimya, amesema tume inasimamia sheria mbili ambazo ni Sheria ya Alama za Bidhaa inayowapa nguvu ya kupambana na bidhaa bandia na Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003 inayosimamia soko kuhakikisha kunakuwa na ushindani wa haki.
“Sheria ya ushindani ina makatazo; unapokuwa mshindani sokoni hupaswi kukaa kikao na mwenzako ambaye ushindani unafanana kibiashara kupanga bei sokoni.
“Kwa washindani ambao wana nguvu kubwa sokoni hawapaswi kuwakandamiza wazalishaji wadogo au washindani wadogo,” amesema Kalindimya.

Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA mkoani Geita.