SERIKALI KUFIKISHA MAJI KATA ZILIZOBAKI KILWA
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi wa Kata za Limaliyao na Kivinje jimbo la Kilwa Kusini kuwa serikali inaendelea na jitihada kuhakikisha inawafikishia huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.
Amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kilwa Masoko mara baada ya kupokea maombi kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo, Ally Kasinge, ambaye amesema kata hizo bado hazijafikiwa na huduma ya majisafi.

Na Mwandishi Wetu, Lindi

"Mheshimiwa Mbunge maendeleo ni safari, tumeshaianza safari kwenye kata nyingine, lengo letu ni kuhakikisha hizo kata mbili zilizobaki pia zinafikiwa na huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza," amesema Rais Samia.
Rais Samia amesisitiza kuwa ahadi ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza inamfikia kila mwananchi.
Rais Samia yupo katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Kusini ambapo Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameshiriki katika ziara hiyo katika kuhakikisha maagizo na maelekezo yote yanayotolewa na Rais yanatekelezwa kwa wakati na viwango.