RUANGWA WASHUKURU KWA MIRADI YA MAJI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Rais Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Maonesho Kilimahewa, Ruangwa, mkoani Lindi.

Na Mwandishi Wetu, Lindi

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu fedha nyingi ambazo zimewezesha utekekezaji wa miradi ya maji.

Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa ametoa pongezi hizo kwa Rais Samia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Maonesho Kilimahewa, Ruangwa mjini.

Amesema kupitia Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, zaidi ya Sh bilioni 184 zilitolewa na kuwezesha utekelezaji wa mradi ambao umehudumia Mji mdogo wa Nyangao hadi Ruangwa na hivyo kuwezesha zaidi ya vijiji 55 kupata huduma ya maji.

Amesema Wizara ya Maji imetekekeza miradi mingi na inaendelea na utekekezaji ambao unatoa matumaini kwa wananchi wa Ruangwa.

Ameishukuru Wizara ya Maji kwa usimamizi mzuri wa fedha kwani miradi iliyotekekezwa inathibitisha viwango na ubora unaostahili.

Rais Samia yuko katika ziara ya kikazi mikoa ya kusini ambapo Septemba 17 ameanza ziara katika Mkoa wa Lindi.
Powered by Blogger.