‘MAONYESHO MADINI YAMEPUNGUZA MATUMIZI YA ZEBAKI’
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la EPZA, Geita. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi na Kushoto ni Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele. (Picha na Nora Damian).
Na Nora Damian, Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigela amesema Maonyesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yamepiga hatua kwa kuwezesha kujengwa kwa miundombinu 10 ya kuchenjua dhahabu (CIP).
Hatua hiyo imewezesha kupungua kwa matumizi ya kemikali ya mekyuri (zebaki) ambayo inatajwa kuwa na madhara makubwa ya kiafya kwa binadamu na kuharibu mazingira.
Tanzania imetia saini ya ukomo wa matumizi ya zebaki ifikapo 2024 na ni miongoni mwa nchi 139 duniani zilizoingia Mkataba wa Minamata unaolenga kupunguza matumizi ya kemikali hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21,2023 katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Usindikaji Nje (EPZA) Mjini Geita yanakofanyika maonyesho hayo, amesema miundombinu hiyo imejengwa baada ya maonyesho ya 2021 na 2022.
“Maana yake wananchi wameanza kuelewa umuhimu wa CIP, ukitumia faida zake ni kubwa sana, ukitumia mercury (zebaki) unakamata dhababu kwa asilimia 25 lakini ukitumia CIP unakwenda mpaka asilimia 99 dhahabu iliyoko kwenye mchanga yote unaichukua,” amesema Shigela.
Amesema mbali ya Serikali kupata mapato kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wa Mkoa wa Geita wanafaidika kwa kiasi kikubwa.
Kwa mujibu wa Shigela, idadi ya washiriki imeongezeka kutoka 250 mwaka 2022 hadi kufikia zaidi ya 400 mwaka 2023 zikiwemo pia nchi za Burundi, China, India, Kenya, Malawi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
“Mwitikio ni mkubwa, wananchi pamoja na wachimbaji wameelewa maana ya maonyesho. Pia wafanyabiashara hasa makampuni yanayojihusisha na utafiti wa madini, uchenjuaji, uchimbaji na teknolojia ya uongezaji thamani wameona umuhimu wa kushiriki.
“Kama mkoa tumeweka mazingira mazuri ya kupokea makampuni yote yanayojihusisha na utafiti wa madini ili waje na teknolojia mpya na rahisi itakayowawezesha wachimbaji wadogo kufaidika,” amesema.

Banda la Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ambao ni wadhamini wakuu wa maonyesho hayo. (Picha na Nora Damian).
Kuhusu mabanda ya kudumu amesema wameanza mchakato wa kutengeneza ‘master plan’ na kuzitaka sekta binafsi kujitokeza ili waonyeshwe maeneo ya kujenga.
Mwaka 2021 wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifunga maonyesho ya nne aliagiza kujengwa mabanda ya kudumu ili kuwawezesha washiriki kutotumia gharama kila mwaka.
Maonyesho hayo yanayotarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 23 na Naibu Waziri Mkuu, Dk. Doto Biteko na kufungwa Septemba 30 na Rais Samia Suluhu Hassan yana kaulimbiu; Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira.
Wadhamini wakuu wa maonyesho hayo ni Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML).