MEKYURI INAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME, KUHARIBU MIMBA
Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii wa NEMC, Lilian Mkambuz, akizungumza wakati wa mafunzo ya kuongeza uelewa wa madhara ya matumizi ya mekyuri kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.
Na Nora Damian, Geita
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeeleza athari za kimazingira na kibinadamu kutokana na matumizi yasiyo salama ya mekyuri (zebaki) katika kuchenjua dhahabu ikiwemo kupungua kwa nguvu za kiume.
Tathmini inaonyesha wachimbaji wadogo wa dhahabu hutumia tani 13.2 hadi 24.4 ya mekyuri kwa mwaka katika kuchenjua dhahabu.
Madhara hayo yameelezwa Septemba 21,2023 wakati wa mafunzo ya kuongeza uelewa wa madhara ya matumizi ya mekyuri kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita ambapo NEMC imetumia Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini kutoa elimu kwa wachimbaji hao.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Dk. Berfina Igulu kutoka NEMC ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Mekyuri kwa Wachimbaji Wadogo (EHPMP), amesema matumizi ya mekyuri yatafikia kikomo hapa nchini ifikapo 2025.
Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Matumizi ya Mekyuri kwa Wachimbaji Wadogo, Dk. Berfina Igulu, akizungunza wakati wa mafunzo ya kuongeza uelewa wa madhara ya matumizi ya mekyuri kwa wachimbaji wadogo mkoani Geita.
“Kupitia mradi huu tutaweza kupitia sheria na kanuni zilizopo na kuziboresha kwa kuingiza vipengele vitakavyowezesha usimamizi thabiti wa uingizaji, utunzaji, utumiaji wa zebaki nchini,” amesema Dk. Igulu.

Madhara mengine yatokanayo na mekyuri ni kuathirika kwa mfumo wa fahamu, figo, kuchanganyikiwa, kupoteza kumbukumbu, msongo wa mawazo, kupoteza uwezo wa macho kuona vizuri, kuharibika kwa mimba, watoto kuzaliwa na mtindio wa ubongo na mengine.
Mwenyekiti wa Wanawake Wachimbaji Madini Mkoa wa Geita, Asia Masimba, amekiri kuwa mekyuri inawaathiri na kusisitiza wakipata mbadala wa kemikali hiyo wataachana nayo.
“Ni kweli tunaumia kutokana na mekyuri, ukiangalia mikono ya wale wanaosugua ile mekyuri wamekatika viganja maana yake wameathirika tayari…njaa ndio inatufanya tushike zebaki lakini wakituletea mbadala wake kila mmoja ataachana nayo,” amesema Masimba.
Wachimbaji wadogo kutoka maeneo mbalimbali mkoani Geita wakifuatilia mafunzo ya kuongeza uelewa wa madhara ya matumizi ya mekyuri.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari za Mazingira na Jamii, Lilian Mkambuz, amesema wanakusudia kuanzisha ofisi ya kanda itakayokuwa katika Mkoa wa Geita kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
“Sekta ya madini inatumia teknolojia lakini kwa wachimbaji wadogo kuna matumizi ya zebaki ambayo yanaleta changamoto katika mazingira na afya za watumiaji. Ili sekta hii iweze kuwa endelevu mradi huu uliweza kufikiriwa na kuanzishwa,” amesema Mkambuz.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Maghembe, ambaye alifungua mafunzo hayo amesema yatasaidia kuwajengea uelewa wachimbaji katika uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na utunzaji wa mazingira.
“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwa kuzingatia kuwa ongezeko la wachimbaji wadogo nchini linakwenda sambamba na ongezeko la uharibifu wa mazingira, matumizi ya kemikali ya zebaki yanaleta athari katika afya ya jamii na uharibifu wa mifumo ya ikolojia,” amesema Maghembe.
Serikali kupitia NEMC inatekeleza mradi huo katika mikoa saba yenye idadi kubwa ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ambayo ni Mwanza, Geita, Shinyanga, Songwe, Singida, Mara na Mbeya.