RITA YASISITIZA WATOTO WAPEWE MAJINA YA WAZAZI HALISI
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu (Kulia), akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mkazi wa Geita, Manasseh Elias, katika Maonyesho ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili, mkoani Geita. Katikati ni Wakili wa Serikali kutoka Rita, Salvius Rwechungura.
Na Nora Damian, Geita
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (Rita) umesisitiza majina wanayopewa watoto yawe ya wazazi halisi ili kulinda haki zao na kuepusha migogoro ya kifamilia.
Akizungumza Septemba 26,2023 na The Page Media, Wakili wa Serikali kutoka Rita, Salvius Rwechungura, amesema mtoto ana haki zake kisheria na anastahili urithi wa baba yake.
Wakili huyo alikuwa akizungumza katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita Rita ambapo wanatoa huduma mbalimbali zikiwemo za vyeti vya kuzaliwa.
“Inaweza kutokea mtu akaweka jina kulingana na mtu atakayeona atatunza mtoto lakini akijua kwamba si mzazi wake, tunasisitiza watakaowekwa kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto wawe ni wazazi kibaiolojia, asipandikizwe mtu kwa malengo fulani ambapo kesho na kesho kutwa anaweza asiwepo.
“Mzazi anafahamu baba wa mtoto ni nani, kama mtoto ni wa fulani hawezi kubadilika, tunamshauri aweke jina sahihi kuepusha migongano baadaye… anaweza akamsaidia kwa utaratibu mwingine lakini haina haja ya kubadilisha jina,” amesema Rwechungura.

Wakili wa Serikali kutoka Rita, Salvius Rwechungura (Katikati), akimweleza Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu, huduma wanazotoa katika Maonyesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili, mkoani Geita.
Amesema jina ndiyo hatua ya kwanza ya kumtambulisha mtu katika jamii na kumwezesha kupata haki nyingine lakini kukiwa na utata anaweza kuchelewa au kukosa kabisa haki husika.
“Tunasisitiza watakaowekwa kwenye vyeti vya kuzaliwa vya watoto wawe ni wazazi kibaiolojia, asipandikizwe mtu kwa ajili ya malengo fulani ambapo kesho na kesho kutwa anaweza asiwepo,” amesema.
Wakili huyo amesema pia kabla mtoto hajazaliwa wazazi husika wanapaswa kukubaliana jina kuepuka kuchelewa kumsajili.
“Wengine wanachelewa kusajili kwa sababu ya kuwa na mjadala mrefu kuhusu majina, wamuite jina la babu, mjomba kwahiyo ni vema watu wakawa na utaratibu mtoto kabla hajazaliwa mnakubaliana jina mtakalompa kama akiwa wa kike au wa kiume,” amesema Rwechungura.