KANYASU AIPA KONGOLE FCC MAPAMBANO BIDHAA BANDIA
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu, akimsikiliza Ofisa Mkaguzi na Mfuatiliaji wa Bidhaa Bandia Kanda ya Ziwa, Mgasi Kalindimya, alipotembelea kliniki ya biashara inayojumuisha taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo FCC. Kliniki hiyi ipo katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili, mkoani Geita.
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu ameipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa shughuli mbalimbali inazozifanya ikiwemo kupambana na bidhaa bandia sokoni.
Kanyasu ametoa pongezi hizo Septemba 26,2023 baada ya kutembelea kliniki ya biashara inayojumuisha taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo FCC katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
“Mnafanya kazi nzuri na kila mtu anaona, naomba muendelee kutoa elimu katika jamii ili iweze kuelewa shughuli mnazozifanya kama za masuala ya ushindani na bidhaa bandia kwa sababu bado watu wengi hawana uelewa wa kutosha,” amesema Kanyasu.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, amesema wamekuwa wakishiriki kwenye maonesho hayo na mengine ili kutoa elimu kwa umma uweze kukitambua chombo hicho na shughuli wanazozifanya za kulinda ushindani katika biashara na kumlinda mlaji.
“Tunakuhakikisha majukumu tuliyonayo kisheria yanatekelezwa kwa ufanisi, tunahakikisha kwamba mlaji na mtumiaji wa bidhaa analindwa na kudhibiti uwepo wa bidhaa bandia katika soko la nchi yetu.
“Tunajua mheshimiwa unashiriki vikao vya kamati ya ushauri ngazi ya mkoa na halmashauri yako na wabunge wengine pia watusaidie kutupatia nafasi ya kuja kutoa elimu,” amesema Nsajigwa.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, akimweleza Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu, shughuli za tume hiyo baada ya kutembelea kliniki ya biashara inayojumuisha taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo FCC katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika viwanja vya EPZA Bombambili, mkoani Geita.
“Tunatoa elimu tunawaasa wasikimbilie kwenye taasisi za mitaani wa sababu kuna kitu kinaitwa kausha damu wengi wanakuja bandani wanalalamika sana, wamekopa wananyang’anywa mali zao, sisi tunawashauri waende kwenye taasisi zinazotambulika kisheria,” amesema Kalindimya.
Aidha amewataka wazalishaji kufanya kazi kwa karibu na tume hiyo ili kuhakikisha bidhaa bandia haziingii sokoni na kusisitiza kuzalisha bidhaa ambazo hazitaigwa na wengine.
Katika maonesho hayo tume hiyo inatoa elimu kwa umma jinsi ya kutambua bidhaa bandia na kuwataka Watanzania kuchukua hatua kujiepusha nazo kwa sababu zina athari kiafya, zinahatarisha usalama wa mali na maisha na zinaongeza umaskini kwa kulazimu kuzinunua mara kwa mara kutokana na kuharibika haraka.
Na Nora Damian, Geita
Mbunge wa Geita Mjini, Costantine Kanyasu ameipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa shughuli mbalimbali inazozifanya ikiwemo kupambana na bidhaa bandia sokoni.
Kanyasu ametoa pongezi hizo Septemba 26,2023 baada ya kutembelea kliniki ya biashara inayojumuisha taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo FCC katika Maonesho ya Sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mkoani Geita.
“Mnafanya kazi nzuri na kila mtu anaona, naomba muendelee kutoa elimu katika jamii ili iweze kuelewa shughuli mnazozifanya kama za masuala ya ushindani na bidhaa bandia kwa sababu bado watu wengi hawana uelewa wa kutosha,” amesema Kanyasu.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa FCC, Nsajigwa Wilfred, amesema wamekuwa wakishiriki kwenye maonesho hayo na mengine ili kutoa elimu kwa umma uweze kukitambua chombo hicho na shughuli wanazozifanya za kulinda ushindani katika biashara na kumlinda mlaji.
“Tunakuhakikisha majukumu tuliyonayo kisheria yanatekelezwa kwa ufanisi, tunahakikisha kwamba mlaji na mtumiaji wa bidhaa analindwa na kudhibiti uwepo wa bidhaa bandia katika soko la nchi yetu.
“Tunajua mheshimiwa unashiriki vikao vya kamati ya ushauri ngazi ya mkoa na halmashauri yako na wabunge wengine pia watusaidie kutupatia nafasi ya kuja kutoa elimu,” amesema Nsajigwa.
Ofisa Mkaguzi na Mfuatiliaji wa Bidhaa Bandia Kanda ya Ziwa, Mgasi Kalindimya, amesema wanatumia maonesho hayo kuwaelimisha Watanzania kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ya bidhaa bandia, ushindani sokoni na namna ya kupata mitaji na teknolojia mpya.