‘WATANZANIA WASHIKAMANE NA KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA’


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 
Watanzania wametakiwa kushikamana na kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi anazofanya katika kuleta maendeleo na demokrasia nchini.
 
Wito huo umetolewa leo Agosti 16, 2023 na Katibu wa Chawa wa Mama Wilaya ya Ilala (CHAMATA), Said Tekelo, wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
 
Amesema Rais Samia anafanya kazi kubwa ya kujenga utaifa na kuwafanya watu wajisikie wamoja na washikamane bila kujali tofauti zao za makabila, dini, mahali wanapotoka na kadhalika.
Katibu wa Chamata Wilaya ya Ilala, Said Tekelo.

“Ili kuimarisha utangamano wa Tanzania nzima ni lazima tuwe wamoja, tushikamane. Sisi tutahakikisha tunamsemea mheshimiwa rais kwenye miradi yote aliyokwishaifanya, miradi ya kimkakati ya mingine inayoendelea.
 
“Tunamsemea mheshimiwa rais kwa sababu wako watu wanapotosha kazi njema anazozifanya, sisi tupo kuhakikisha kila kazi njema anayoifanya mheshimiwa rais inatambulika ndani na nje ya nchi,” amesema Tekelo.
 
Amesema Rais Samia anajali utu, hana ukanda wala ukabila na kuwataka Watanzania kuendelea kushikamana na kuiunga mkono Serikali katika shughuli zote inazofanya.
 
Katibu huyo amelaani njama zenye nia ovu ya kwenda kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vikundi vichache vinavyotaka kuhatarisha amani ya nchi.
 
“Mheshimiwa Rais amejipambanua kitaifa na kimataifa kuwa yeye ni mwanademokrasia, sasa kuruhusu demokrasia nchini isiwe chanzo cha watu wachache kutumia uhuru huo kuhatarisha amani ya nchi yetu,” amesema.




Powered by Blogger.