VYAMA 6,000 VYASAJILIWA KIDIGITALI
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Dk. Benson Ndiege, akiangalia Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) unavyofanya kazi baada ya kutembelea banda la tume hiyo kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Na Nora Damian, Mbeya
Vyama vya msingi na vikuu vya ushirika 6,000 kati ya 7,300 vimesajiliwa katika Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) ambao umeanza kutumika mwaka huu.
Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) inatumia Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya kutambulisha mfumo huo kwa wadau wa sekta ya ushirika.
Akizungumza Agosti 6, 2023 Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dk. Benson Ndiege, amesema mfumo huo unafuatilia shughuli zote za vyama vya ushirika.
“Siku za nyuma tulikuwa na changamoto kubwa kwenye usimamizi wa vyama vya ushirika, kumekuwepo na uwazi mdogo na watu wachache kutumia mifumo ambayo siyo wazi kuwaibia wana ushirika,” amesema Dk. Ndiege.
Amesema mpaka sasa wameshapata takwimu za vyama vya ushirika na wanachama wao na kwamba vyama vimeanza kupitisha bajeti zao kupitia mfumo huo.
“Badala ya chama kusafiri kutoka kwenye kituo chake kwenda ofisi ya mrajisi wa mkoa au taifa, anaingiza taarifa kwenye mfumo zinapitishwa na afisa ushirika na mrajisi,” amesema.
Amesema pia kupitia mfumo huo wanatoa leseni za vyama vya akiba na mikopo (Saccos) na nyingine tayari zimeanza kuwasilisha taarifa zake kupitia kwenye mfumo.
Mtendaji huyo amesema wametoa elimu kwa wadau wa sekta hiyo waweze kuuelewa mfumo huo ili iwe rahisi kuutumia.
Amesema mwelekeo wa ushirika ni kuhakikisha Watanzania wengi wanatumia mfumo wa ushirika kwenye shughuli zao za kila siku.
“Mwelekeo wa ushirika ni kuwa na ushirika ambao ni imara zaidi, unafanya kazi kisasa, unatumia mifumo ya kidigitali, unafanya kazi kwa malengo ya kibiashara sio kutoa huduma tu…mwelekeo ni kwamba waanze kuongeza thamani za mazao,” amesema Dk. Ndiege.
Kupitia mfumo huo shughuli zote za vyama vya ushirika kama kuomba bajeti, kufanya mikutano mikuu, kuajiri na mengine yatakuwa yakionekana kwenye mfumo.
“Kwahiyo itatusaidia kukiangalia chama kwa ukaribu zaidi, sio lazima nifike kwenye chama ndipo nijue changamoto yake, naweza nikajua kwa kuangalia tu taarifa zake za mwezi kwenye mfumo,” amesema.
Dk. Ndiege amesema pia kwa kuwa na benki ya ushirika wana ushirika watakuwa na sehemu ya kuwekeza kwani vyama vya ushirika ndio vinaimiliki.
Amesema kupitia Kijiji cha Ushirika ambacho kimekusanya wadau mbalimbali wa sekta hiyo, washiriki wanapata fursa ya kuonyesha shughuli wanazozifanya, kujifunza vitu mbalimbali vitakavyowafanya waongeze tija na kuongeza uzalishaji.