'TEMBELEENI BANDA LA TPHPA KUPATA ELIMU SAHIHI YA VIUATILIFU'




Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania, Profesa Joseph Ndunguru amewataka wananchi wa nyanda za juu kusini kutembelea katika banda la mamlaka hiyo kupafa fursa ya kujifunza zaidi.

Profesa Ndunguru ameyasema hayo Agosti 2, 2023 kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Amesema wamejipanga kutoa elimu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu, vinyunyizi, udhibiti wa visumbufu vya mimea, taratibu za uingizaji wa mazao nchini na utoaji wa mazao nje ya nchi, usimamizi wa biashara ya viuatilifu (taratibu za usajili wa viatilifu na biashara za viuatilifu.

Pia amesema mamlaka hiyo inatoa elimu juu ya uhifadhi wa bioanuai za mimea, udhibiti wa visumbufu vya mimea kwa kutumia njia za kibaolojia, na udhibiti wa wa visumbufu vya mlipuko.



Mwenyekiti wa kamati ya mandalizi ya Maonesho ya Nanenane 2023 kwa upande wa mamlaka hiyo, Dk. Mujuni Kabululu, amewaomba wananchi kutembelea kupafa fursa ya kukutana na wataalum ambao wanatoa elimu na kupokea changamoto mbalimbali za wakulima.
Powered by Blogger.