ST MARY'S MZUMBE YADHAMIRIA KUFAULISHA KWA ASILIMIA 100
Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, Dk. Rose Rwakatare, akizungumza wakati wa mahafali ya Darasa la Saba na Awali ya Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial iliyopo Mzumbe Morogoro.
Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial iliyopo Mzumbe mkoani Morogoro imeweka malengo ya kupata ufaulu wastani wa 273 katika mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na wanafunzi 47 na kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya 370.
Akizungumza Agosti 19, 2023 wakati wa mahafali ya Darasa la Saba na Awali ya Shule ya shule hiyo Mwalimu Mkuu, Elphas Kavusia, amesema wamewaandaa watoto vizuri hivyo wanatarajia watafanya vema.
"Tumewaandaa watoto vizuri, tumefanya mitihani mingi ya kujipima ambayo watoto wetu wamefanya vizuri, kwahiyo tunatarajia wanafunzi wote watafaulu mtihani wa taifa," amesema Kavusia.
"Tunawashirikisha watoto katika utunzaji mazingira, tumeanzisha shamba darasa la mbogamboga ambapo wanajifunza kilimo kwa vitendo.
"Mwakani tunatarajia kuanzisha somo la Kichina na Kifaransa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya ulimwengu," amesema Mwalimu Kavusia.Wahitimu wa darasa la saba
"Haikuwa rahisi kufika hapa, lakini tumefika kwa msaada wa walimu wetu na Mungu. Kumcha Mungu na kujituma ndio msingi wa mafanikio...naamini tutafanya vema kwenye mtihani wa taifa," amesema Selina ambaye pia alitunukiwa cheti cha kiongozi bora.
Na Nora Damian, Morogoro
Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial iliyopo Mzumbe mkoani Morogoro imeweka malengo ya kupata ufaulu wastani wa 273 katika mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi.
Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na wanafunzi 47 na kwa sasa ina wanafunzi zaidi ya 370.
Akizungumza Agosti 19, 2023 wakati wa mahafali ya Darasa la Saba na Awali ya Shule ya shule hiyo Mwalimu Mkuu, Elphas Kavusia, amesema wamewaandaa watoto vizuri hivyo wanatarajia watafanya vema.
"Tumewaandaa watoto vizuri, tumefanya mitihani mingi ya kujipima ambayo watoto wetu wamefanya vizuri, kwahiyo tunatarajia wanafunzi wote watafaulu mtihani wa taifa," amesema Kavusia.
Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, Dk. Rose Rwakatare, akimpongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial, Elphas Kavusia, wakati wa mahafali ya awali na darasa la saba ya shule hiyo.
Amesema pia wanafanya vizuri kwenye michezo na kwamba wana mpango wa kuongeza michezo zaidi kwa kuwa na uwanja wa kikapu na wavu ili kubaini uwezo wa watoto katika nyanja mbalimbali.
"Tunawashirikisha watoto katika utunzaji mazingira, tumeanzisha shamba darasa la mbogamboga ambapo wanajifunza kilimo kwa vitendo.
"Mwakani tunatarajia kuanzisha somo la Kichina na Kifaransa ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya ulimwengu," amesema Mwalimu Kavusia.
Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial.
Mkurugenzi wa Shule za St Mary's, Dk. Rose Rwakatare, amesema wanaendeleza maono ya mama yao Dk. Getrude Rwakatare ya kukuza sekta ya elimu nchini ambapo wamejipanga kuwa na mtandao wa shule hizo Tanzania nzima.
"Tunawashukuru Watanzania kwa kuendelea kutuamini na kutuletea watoto, tunaiunga mkono Serikali katika kukuza sekta ya elimu nchini. Mwaka jana tulianzisha shule mpya mbili na malengo yetu ni kuweka mtandao wa shule zetu Tanzania nzima," amesema Dk. Rose.
Dk. Rose ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Morogoro amewaasa wazazi kuwa karibu na watoto wao na kuwafunza maadili mema kuepuka mmonyoko wa maadili.
"Nawaomba wazazi tuangalie watoto wetu kwa karibu, mambo mengi yanaendelea kwa sababu hatuko karibu nao, mtenge muda wa kuongea na watoto, ukimfanya rafiki atakuambia mengi.

Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero, Said Nguya, akizungumza wakati wa mahafali ya Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial.
"Dunia imeharibika, kuna wimbi la mambo mengi machafu, kuna ushoga, usagaji, sisi kama wazazi kuanzia nyumbani tuwakemee, tuangalie utumiaji wa simu kwa watoto wetu, mambo mengine wanaiga, sisi sio Wazungu, sisi ni Waafrika tuna mila na desturi zetu," amesema.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya Mvomero ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mvomero, Said Nguya, amewaasa wanafunzi hao kujitahidi kufanya vema katika mtihani wa taifa ili waweze kufikia ndoto zao.
"Tunatarajia tunapoangalia matokeo na shule bora tusiyachoshe macho, tunataka tuwaone kuanzia juu hivyo, mnalo jukubwa. Ninyi mkifaulu hata mimi kwa nafasi yangu nahesabu ni ushindi," amesema Nguya.

Selina Kadilo akifurahia baada ya kuhitimu darasa la saba wakati wa mahafali yaliyofanyika katika Shule ya St Mary's Rwakatare Memorial, Morogoro.
Mmoja wa wahitimu wa darasala saba, Selina Kadilo, ameushukuru uongozi wa shule kwa malezi mazuri na kuahidi kuwa watafanya vema katika mtihani wa taifa.