RAIS SAMIA: NIMEAMUA KUNYAMAZA KIMYA
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania yaliyofanyika jijini Arusha.
Na Nora Damian
Rais Samia Suluhu Hassan amesema amesikia yote yanayojadiliwa nchini lakini ameamua kukaa kimya na ataendelea kufanya hivyo.
Amewahakikishia Watanzania kuwa hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa, au kuliuza au kuharibu amani na usalama uliopo.
Rais Samia ameyasema hayo Agosti 21, 2023 jijini Arusha wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
"Baba Askofu Shoo (Mkuu wa KKKT) nimeyasikia yote uliyoyasema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa taifa letu. Niliamua kunyamaza kimya na naendelea kunyamaza kimya.
"Nawahakikishia hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza taifa hili, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye taifa hili...hayo yatoshe kuwa ni ujumbe wangu kwenu," amesema Rais Samia.
Aidha amesema Serikali imejidhatiti kuimarisa misingi ya utawala bora inayozingatia sheria, demokrasia na maadili ya Mtanzania ndiyo maana inatekeleza falsafa nne ambazo ni maridhiano, kustahimiliana, mabadiliko na kujenga upya.
"Katika ile 'R' ya kwanza ya maridhiano nilipata ushirikiano mkubwa sana wa kaka zangu baba Askofu Shoo na baba Askofu Bangonza. Walinisaidia sana nikaweza kupiga hatua," amesema.
Rais Samia amesema Serikali inatambua mchango wa kanisa hilo katika kuwahudumia Watanzania na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo.
Amesema miaka 60 imekuwa yenye manufaa si tu kwa waumini wa KKKT bali kwa Watanzania wote na kuwataka viongozi wapya watakaochaguliwa kuendeleza misingi mikuu ya kuanzishwa kwake.

"Wakati nikioneshwa kazi zinazofanywa na kanisa nimeoneshwa misingi mikuu ya kanisa, niwaombe viongozi watakaochaguliwa kuendeleza misingi mikuu ya kanisa....misingi ile ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo mpaka leo tunajivunia," amesema Rais Samia.
Aidha amesema Serikali itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zinazojitokeza kupitia sera ya PPP ili kuwahudumia wananchi ipasavyo.
ASKOFU SHOO
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Fredrick Shoo, amesema suala la uwekezaji wa bandari linahitaji hekima kubwa na kumpongeza Rais Samia kwa kukaa kimya dhidi ya mijadala mbalimbali inayoendelea.
“Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi umekaa kimya, lakini kimya chako hicho si kwamba hufanyi kazi, jambo hili linahitaji hekima kubwa na sisi tunakuombea kwa Mungu ili hekima itumike kuliendea jambo hili muafaka upatikane,” amesema Dk. Shoo.

Amesema wanaunga mkono juhudi zitakazowawezesha wananchi kujipatia maendeleo kwa njia ya utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu na kuruhusu demokrasia ya kweli miongoni mwa wananchi na vyama vya siasa.
"Mheshimiwa Rais kanisa liko pamoja na wewe, tutaendelea kukuombea na kukuunga mkono katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu kwa masilahi mapana ya nchi yetu.
"Umeweka wazi msimamo wako na tumeona watu wakiwa huru na kueleza maoni yao, ni matumaini yetu iwapo watendaji wataielewa vema nia yako njema nchi yetu itaendelea kuwa yenye amani na mshikamano jambo ambalo litaimarisha umoja wa kitaifa.
"Kazi yetu viongozi wa dini ni kuwaombea ili mtimize wajibu wenu lakini pia mjue pale ambapo tunaona hapajaenda sawa hatutaacha kuwaona na hata kuwashauri na kama kuna mahali pa kukemea tutakemea...ikifika kwenye hatua hiyo tusiambiwe msichanganye dini na siasa," amesema Dk. Shoo.
Kwa mujibu wa Askofu Shoo, kanisa hilo lilianza kama jamii ya waumini 500,000 na sasa wako zaidi ya milioni 8.