MRADI WAOKOA WATOTO 21,000 UZALISHAJI TUMBAKU
Ofisa Elimu Kazi Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Honesta Ngolly (aliyekaa), akitoa elimu kwa wananchi katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya.
Na Nora Damian, Mbeya
Zaidi ya watoto 21,000 wa Mikoa ya Mbeya, Songwe na Tabora wameokolewa kutoka katika shughuli za uzalishaji wa tumbaku na kuingizwa katika shughuli mbadala baada ya kumaliza masomo.Kifungu cha 5 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini kinazuia ajira za mtoto ambapo chini ya miaka 18 haruhusiwi kuajiriwa isipokuwa kati ya miaka 14 mpaka 17 anaweza kupewa kazi ambazo zinamuandaa kupata ujuzi wa aina mbalimbali ambazo hazina madhara.
Akizungumza Agosti 5, 2023 kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, Meneja Mradi wa Kupambana na Ajira za Watoto (PROSPER) Katika Mkoa wa Tabora, Fredrick Malaso, amesema ulianza mwaka 2011 ambapo unatekelezwa katika Wilaya za Urambo, Kaliua na Sikonge (Tabora), Songwe (Songwe) na Chunya (Mbeya).
Amesema mradi huo umejikita katika kuijengea uwezo jamii ili kuinua uchumi wa familia zinazojihusisha na uzalishaji wa tumbaku vijijini na kuhakikisha hawatumikishi watoto.
“Tunatoa elimu ili wazazi wasitumikishe watoto kwenye shughuli za uzalishaji wa tumbaku na badala yake tunawapa elimu ya kufanya shughuli mbadala za kuongeza kipato ili kuhakikisha wanawapa watoto fursa ya kupata elimu na kuwapatia huduma za msingi kama vile afya na mahitaji ya shule,” amesema Malaso.
Kwa mujibu wa Malaso, watoto waliookolewa walipelewa shule na wengine walipatiwa elimu ya ujasiriamali na ufundi stadi na sasa wanafanya shughuli nyingine hawajihusishi na uzalishaji wa tumbaku ambao ni hatarishi.
Amesema pia kwa mradi ulioanza 2021 ukitarajiwa kukamilisha mwishoni mwa 2023 walikusudia kuwafikia watoto 2,200 lakini mpaka sasa wamewafikia 2,300.
Ofisa Elimu Kazi Mwandamizi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Honesta Ngolly, amesema wanasimamia utekelezaji wa sheria za kazi nchini kwa kuwaelimisha waajiri, wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi kuzingatia sheria.
“Sekta ya kilimo imezalisha ajira nyingi lakini ipo changamoto ya wafanyakazi yaani waajiri kuajiri watoto chini ya umri wa miaka 18 na wengine wameajiri chini ya miaka 14, kwenye maonesho haya tumekutana na wakulima wengi, wafugaji, makampuni ya ununuzi wa mazao.
“Kwetu ni wadau muhimu kwa sababu bado sekta ya kilimo ndiyo inaongoza katika ukuzaji wa uchumi wa nchi yetu, hivyo tunashirikiana katika kuhakikisha kwamba sekta hii inakuwa imara, haina migogoro na kuweza kuzalisha ajira zaidi,” amesema Ngolly.