MRADI WA VANILA WAZINDULIWA DODOMA, KUGHARIMU BILIONI 30



Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Vanila international, Simon Mkondya.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kampuni ya Vanila International Limited imezindua mradi wa kilimo hicho mkoani Dodoma utakaogharimu zaidi ya Sh bilioni 30.

Uzinduzi huo uliofanyika Julai 22, 2023 katika shamba kitalu (green House) umeambatana na utoaji elimu kwa wananchi wa eneo hilo kuhusu kilimo cha vanila kinachotumia teknolojia ya kisasa.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya Vanila international, Simon Mkondya, amesema mradi huo utatekelezwa katika Kitongoji cha Zamahero Kata ya Mayamaya Wilaya ya Bahi.

Vanila ikiwa shambani.

Aidha amesema shamba kitalu hilo lenye ukubwa wa hekta 125 lipo kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara kuu iendayo Arusha.

"Uwekezaji huu unakuja baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia kilimo hiki Zanzibar," amesema Mkondya.
Powered by Blogger.