CHONGOLO: MKATABA BANDARI UNAREKEBISHIKA
Na Nora Damian
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo, amesema mkataba wa uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam unarekebishika na kuielekeza Serikali ichukue maoni yenye dhamira njema ili kuleta tija.
Amesema dhamira ya CCM ni kuhakikisha kinapata fedha za kutosha kwenye kila chanzo muhimu ili zisaidie kuharakisha utekelezaji wa ilani na kutatua changamoto za wananchi.
Chongolo ameyasema hayo leo Julai 29,2023 wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Pakers, Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na viongozi wa Mikoa ya Pwani na Morogoro.
“Wengine wanaita mkataba, wengine wanaita makubaliano, lakini kisheria hayana tofauti, makubaliano si msaafu, kurekebishwa neno, sentensi au maana inawezekana.
“Kama kuna mtu ana mstari ambao ukiwekwa utaleta maana nzuri alete tutoke na kitu bora ambacho kikienda kutekelezwa kitatuongezea tija kubwa, masilahi ya nchi yatakuwa yamelindwa na tutatekeleza ilani kwa kasi zaidi,” amesema Chongolo.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete, amesema Tanzania inashindana na nchi jirani ambazo zimeizidi kwa kila kitu hali inayosababisha baadhi ya wafanyabiashara kuacha kuitumia Bandari ya Dar es Salaam na kutumia nyingine.
“Magati tunayo 12, wenzetu wa Mombasa wana magati 28, Afrika Kusini wana magati 58, katika magati 12 tuliyonayo meli zinazoweza kushusha kwa wakati mmoja ni tisa peke yake…mfanyabiashara anaweza asipitishe bidhaa zake kwa sababu magati machache na vifaa hatuna vya kutosha,” amesema Mwakibete.
Sehemu ya wakazi wa Dar es Saalam waliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Pakers, Kawe.
Mwanasiasa Mkongwe, Stephen Wasira, amesema bandari ni mpaka kati ya Tanzania na nchi nyingine hivyo hakuna anayeweza kuiuza.
“Mwaka 1979 tulipigana vita vya Kagera kwa sababu sehemu ya mpakani ilichukuliwa na adui, sasa kama unaweza kupigana kwa ajili ya kipande cha ardhi ya Kagera utauzaje bandari?” amehoji Wasira.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Silaa, amesema maoni bado yanapokelewa na kutaka kila Mtanzania mwenye maoni ambayo anaamini yataboresha ayawasilishe Serikalini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo, amesema mkataba huo unarekebishika kwani ibara ya 22 inaruhusu marekebisho hivyo Serikali itazingatia maoni yanayotolewa na kuyafanyia kazi.
“Mkataba huu si vitabu vitakatifu, Serikali imesaini mkataba, mikataba yote duniani huwa inarekebishika na katika mkataba huu ipo ibara ya 22 ambayo inaruhusu marekebisho…kwahiyo Serikali haina tatizo na wataalam na Watanzania wenye nia njema,” amesema Profesa Mkumbo.