JESSICA MSHAMA AWAFUNDA MABINTI SAFARI YA UONGOZI

KATIBU wa Uhamasishaji na Chipukizi wa UVCCM, Jessica Mshama amewafunda mabinti kuhusu safari ya uongozi huku akiwataka kuongeza juhudi katika mapambano yao kufikia ndoto zao za uongozi.

Jessica ameyasema hayo alipozungumza na mabinti wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) Kampasi ya Mlimani alipofika kwa ajili ya mafunzo.

Amewataka mabinti kuweka nia thabiti na wajipambanue wafanikiwe katika uongozi kwani si njia rahisi; ni safari inayohitaji maandalizi na kujifunza kila siku watumie fursa za mtandao kujifunza kutoka kwa waliowatangulia wasome, wajielimishe na wajiifunze jinsi ya kuvuka changamoto kwa ustadi na uimara."Jitengenezee fursa nje ya siasa, jitahidi kuwa na 'side hustle' inayokuingizia kipato. Chagua biashara au shughuli ambayo unaweza kuifanya kwa ujasiri na bidii. Anza leo, hata kama ni kidogo na uifanye kwa makini. Fursa hazisubiri, zipange na uzitekeleze," amesema.

Amewahimiza mabinti kuchagua marafiki wanaowachochea, marafiki wana jukumu kubwa katika mafanikio, kuchagua marafiki wanaokupa changamoto za kiakili, wanaokushauri na wanaokuhamasisha kufikia malengo.

"Vijana tupiganie ukombozi wetu wa kifikra, sasa ni wakati wa vijana wa Tanzania kujitokeza na kupigania ukombozi wetu wa kifikra. Tuwe wabunifu, tuchangamke, na tuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika kujenga mustakabali bora. Jitokeze kujiandikisha kama mwanachama wa CCM ikiwa bado hujafanya hivyo, na tuungane kuhakikisha tunachagua viongozi bora.

Vilevile amewataka kupiga kura kwa kuwa ni haki yako ya msingi inayolindwa na katiba kwani ni silaha ya kubadilisha mustakabali wa taifa hivyo, wajitokeze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaostahili kuongoza.

Powered by Blogger.