WATUMISHI WATAKIWA KUTINGATIA TARATIBU ZA MANUNUZI KUEPUSHA MIANYA YA RUSHWA

Na Mwandishi Wetu, Tabora

Watumishi kutoka taasisi mbalimbali wametakiwa kuzingatia taratibu za manunuzi ili kuepusha mianya ya rushwa na kuendelea kujenga uchumi wa nchi imara kwa manufaa ya taifa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi kutoka taasisi mbalimbali kuhusu matumizi ya Mfumo wa NeST ambayo yamefanyika Aprili 7 hadi 11,2025 mkoani humo.

Amesema mafunzo hayo yamekuwa ya kipekee kwa sababu yamejikita katika moduli mpya na muhimu kwa maboresho ya michakato ya ununuzi wa umma nchini ambapo Mfumo wa NeST unaendelea kuboresha uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma."Mara nyingi tunasikia mfumo unachelewesha lakini mimi nasema mifumo haicheleweshi, mifumo hii imekuja kwa ajili ya kurahisisha kazi zetu, ninyi wataalamu wetu mpo hivyo muiangalie na tujitahidi kuwa waadilifu ili tuache kusingizia mfumo,”amesema Chacha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhandisi Deusdetith Katwale, amesema mafunzo hayo ni mwendelezo wa jitihada za serikali katika kuhakikisha changamoto za ununuzi ndani ya taifa ziwe zinashughulikiwa kimifumo ili kuendana na teknolojia inayozidi kushika kasi nchini.

“Sasa hivi serikali inashika kasi kwenye mambo ya kidijitali ambapo zamani tulikuwa tunasema serikali inawasiliana kwa makaratasi tu lakini sasa tunawasiliana kidijitali kwa hiyo ni mwendelezo wa kuhakikisha inakuwa na mifumo imara ya mawasiliano.

"Ni imani yangu kwamba mafunzo yaliyofanyika yataendelea kuleta chachu na kupunguza mianya ya rushwa katika Serikali yetu," amesemaMkurugenzi wa Idara ya Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri kutoka PPRA Makao Makuu, Winfrida Samba, amesema lengo la mafunzo hayo ni kupata elimu kuhusu Mfumo wa NeST ambapo kuna moduli mbalimbali na nyingine ni mpya zilizopelekea kufanyika mafunzo hayo. 

“Katika mfumo wa NeST tuna moduli mbalimbali ikiwemo usajili ambayo inahusika na wazabuni pamoja na taasisi nunuzi, moduli nyingine ni 'E - tendering' ambayo inahusika na uchakataji wa zabuni.

"Pia tuna moduli ya 'E - contract Management' ambayo inahusika na usimamizi na utekelezaji wa mikataba, tuna 'E - payment' ambayo inahusika na masuala ya malipo lakini pia tuna moduli ndogo ambazo ndizo washiriki wamejifunza zaidi," amesema Samba.


Powered by Blogger.