RAIS SAMIA AMLILIA PAPA FRANCIS
Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko. Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani.
Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote.
Mapema mwaka jana Februari 12,2024 Rais Samia alikutana na Papa Francis na kufanya mazungumzo ya faragha mjini Vatican.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina.

