RAIS SAMIA AIPONGEZA SIMBA KWA USHINDI, KUWAPA MOTISHA
Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.
Simba imeibuka na ushindi huo katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
"Hongera sana kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup).
"Mmeleta furaha kwa mashabiki wenu na Watanzania wote na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu.
"Motisha kutoka kwangu mtaipokea kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ninawatakia kila la kheri," amesema Rais Dkt. Samia.
