NICOLE ATIWA MBARONI TUHUMA ZA UTAPELI

Mwigizaji Joyce Mbaga maarufu Nicole.

Na Mwandishi Wetu, The Page - Dar es Salaam

Jeshi la Polisi limemkamata Mwigizaji Joyce Mbaga maarufu Nicole kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Nicole anatuhumiwa kuwahamasisha watu kuchanga fedha kupitia makundi sogozi (WhatsApp) kwa ahadi ya kupata kiwango kikubwa zaidi baada ya muda mfupi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa Machi 3 mwaka huu na mpaka sasa zaidi ya watu 16 wamejitokeza kulalamika kutapeliwa fedha zao na hatua za kisheria zinaendelea ili aweze kufikishwa mahakamani.

"Tunatoa wito kwa wananchi kuepuka kujiunga na 'ma - group' au link mbalimbali wasizozijua ambazo zinawatamanisha kupata kiwango kikubwa cha fedha halafu wanaishia kutapeliwa," amesema Kamanda Muliro.

Powered by Blogger.