MSAMA AKARIBISHA WADHAMINI TAMASHA LA KUOMBEA UCHAGUZI MKUU
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025, Alex Msama.
Na Nora Damian, The Page
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Kuombea Uchaguzi Mkuu 2025, Alex Msama amesema tamasha hilo litafanyika katika mikoa 26 nchini na kuwaomba wadhamini mbalimbali kujitokeza kudhamini.
Akizungumza na waandishi wa habari amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na kwamba litaanza kwa kufanyika katika Jiji la Dar es Salaam na baadaye kuendelea katika mikoa 26 ya Tanzania.
“Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha tamasha hili kubwa ambalo litafanyika mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia na Mkoa wa Dar es Salaam," amesema Msama.
Amesema kwa sasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na kwamba wakifanikiwa kupata wadhamini tamasha litakuwa halina kiingilio.
Tamasha la kuombea uchaguzi litafanyika hivi karibuni na kuwaunganisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya Tanzania.
