DIWANI LUCY LUGOME AGAWA MITAJI YA KUKU KWA WAJASIRIAMALI

Na Heri Shaaban, (ILALA)

Diwani wa Kata ya Kisukuru wilayani Ilala, Lucy Lugome amewagawia mitaji ya kuku wafugaji 800 wa kata hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Diwani Lucy amesena lengo la kugawa kuku kwa wajasiriamali wa Kisukuru ni ili waweze kujikwamua kiuchumi na wakuze mitaji yao.

"Wananchi wangu 800 nimewapatia mtaji kwa kuwapa kuku wa biashara waweze kujikwamua kiuchumi, kuku hawa wanagaiwa kwa mtu yeyote mjasiriamali bila kujali vyama vyao," amesema Lucy.

Diwani Lucy Lugome amesema anaunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kufungua fursa ambapo amesema kata hiyo ina mitaa mitatu na yote imepata kuku wa biashara. 

Mmoja wa wananchi wa Kisukuru, Christina Gabriel, amempongeza diwani huyo kwa kuwawezesha kiuchumi wanawake, vijana na wajasiriamali mbalimbali kwa kuwapatia mitaji.

Christina amewataka wananchi wa Kisukuru kuunga mkono juhudi za Diwani Lucy Lugome za kuwakwamua kiuchumi na kuwafungulia fursa.

Powered by Blogger.