ARENA MBIONI KUTENGENEZWA, KUGHARIMU SH BILIONI 450

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya Serikali.


Na Nora Damian, The page

Serikali imesema inatarajia kutengeneza Arena kwa ajili ya wasanii na shughuli nyingine za burudani katika eneo la Kawe itakayogharimu Sh bilioni 450.

Kujengwa kwa Arena hiyo itakayokuwa na uwezo wa kuchukua watu 15,000 kutawezesha shughuli za burudani na michezo mingine kuwa na eneo lake tofauti na ilivyo sasa ambapo matukio mengi yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya mpira wa miguu ukiwemo Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Akizungumza leo Machi Mosi, 2025 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema fedha zitakazojenga Arena zinatokana na ziara aliyoifanya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea mwaka jana.

“CAF hawapendezwi tunapotumia uwanja wa Mkapa kwa shughuli ambazo ni nje ya michezo, hata sisi Serikali hatufurahishwi, Arena inakuja eneo lilishaandaliwa itajengwa Kawe na Kijiji cha Filamu kitajengwa Kwala,” amesema Msigwa.


Powered by Blogger.