KAMPUNI YA CCCC KUENDELEA KUJENGA UHUSIANO NA VYOMBO VYA HABARI

Na Mwandishi Wetu, The Page

Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano ya China (CCCC) imesema mwaka 2025 wataendelea kujenga uhusiano na vyombo vya habari ikiwemo kuinua kazi za matangazo kwa kiwango kipya.

Kiongozi wa Kampuni ya CCCC Tawi la Tanzania,Yang Runze, amezungumza hayo alipokutana na vyombo vya habari ikiwemo ambapo walitoa mapendekezo yanayohitajika kuboreshwa kwenye kampuni hiyo.

Amesema vyombo vya habari vimeeleza jinsi walivyotoa taarifa za kampuni hiyo mwaka 2024 na walibainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa."Majadiliano yamefanyika kuhusu mbinu mpya za ushirikiano kwa mwaka 2025 na jinsi ya kuboresha kazi zetu," amesema Runze

Amesema kila mwandishi wa habari alielewa ripoti ya maendeleo ya mwaka 2024 iliyofanywa na kampuni ya CCCC ikiwemo mradi wa uboreshaji wa barabara uliopo Bariadi mkoani Shinyaka hadi Lamadi mkoani Mwanza.

Amesema barabara hiyo zinaunganisha mikoa hiyo miwili ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami pamoja na Bariadi hadi Lamadi umbali wa kilometa 1,300 kutoka jijini Dar es Salaam.Mradi wa kuboresha na kujenga upya barabara kwa kiwango cha lami ambayo awali ilikuwa ya changarawe ina urefu wa kilometa 71.8.

Amesema barabara hiyo ikikamilika itapunguza muda na gharama za usafirishaji na itachangia maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo.

Naye Ofisa Utawala wa kampuni ya CCCC, Alice Charles, amesema Kampuni ya CCCC imekuwa ikitumia faida yake kwa kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii ikiwemo shuleni na kwamba mwaka 2025 wataendelea na utaratibu huo.



Powered by Blogger.