MAMLAKA ZA MAJI NA DHAMANA YA KUFIKISHA MAJI KWA WANANCHI MIJINI

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wizara ya Maji kupitia Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini ndio zenye dhamana ya kuhakikisha huduma za maji safi na usafi wa mazingira zinawafikia wananchi wote katika maeneo ya mijini kwa viwango na ubora unaostahili.

Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira nchini iliyowasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma imeeleza jitahada zilizochukuliwa katika kufikisha huduma hiyo kwa wananchi.Moja ya vipaumbele vilivyoelezwa katika taarifa hiyo ni pamoja na kuongeza kasi katika ujenzi na ukamilishwaji wa miradi ya huduma ya maji na miundombinu ya majitaka pamoja na suala la upotevu wa maji.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Anna Lupembe, amewapongeza watendaji na wataalamu wa Wizara ya Maji na taasisi zake kwa kuendelea kufikisha huduma za majisafi katika maeneo ya mijini na vijijini.



Powered by Blogger.