KAMPUNI YA CCCC YAZIDI KUAMINIWA MRADI WA MWENDOKASI
Na Mwandishi Wetu, The Page
Kampuni ya Ujenzi na Mawasiliano inayomilikiwa na Serikali ya China (CCCC) imeendelea kuaminiwa na kupewa kazi ya kujenga miundombinu ya mradi wa mwendokasi katika Jiji la Dar es Salaam.
Kampuni hiyo ambayo inajenga awamu ya nne ya mradi huo tayari imepewa kazi ya kujenga Karakana ya Simu 2000 na hivi karibuni wataanza kujenga barabara katika eneo la Mbuyuni lililopo Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa Septemba 16,2024 na Ofisa Mipango ya Usafirishaji DART, Nassoro Bwatuta, wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikisherehekea tamasha la Mid - Autumn na kukutana na wadau mbalimbali wanaofanya nao kazi za ujenzi.
"Tupo hapa kwa ajili ya mwaliko wa CCCC ambayo inajenga mradi wa mwendokasi wa awamu ya nne kutoka Posta kwenda Boko Basiaya na kutoka Mwenge kwenda Simu 2000 ambao unajengwa na kampuni tatu za China.
"Wametualika kuja hapa tunashirikiana nao, tunafurahi, tunakunywa na kula nao hivyo, nawaomba tuendelee kutekeleza mradi huu ambao una manufaa makubwa kwa taifa letu," amesema Bwatuta.
Amesema kampuni ya kwanza inajenga kutoka Posta hadi Mwenge, Samnujoma na Ubungo na kampuni nyingine inajenga kuanzia Mwenge mpaka Boko Basiaya.

Pia amesema wamepata uzoefu kwa namna wanavyoendesha shughuli zao za ujenzi, kujumuika na jamii pamoja na viongozi wa Serikali za mitaa, mkandarasi ambaye ni mjenzi, wasimamizi, mwajiri yaani Tanroad na Manispaa ya Ubungo ambao wamewapa eneo la Simu 2000 kwa ajili ya ujenzi wa karakana.
Naye BRT Contractors representative, Gou Xudong, amesema wamekuwa wakishirikiana na Serikali ya Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa barabara za mwendokasi.
Xudong amesema wanahakikisha miradi waliyokabidhiwa wanaijenga kwa ubora na wataitekeleza kwa wakati lengo kutimiza malengo waliyopewa na Serikali ya Tanzania.
"Leo tunafurahi pamoja na wadau wetu wakiwemo DART, Tanroad, wahandisi, ofisi ya halmashauri ya Ubungo pamoja na serikali za mitaa. Tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali kwenye jamii inayotuzunguuka," amesema Xudong.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni Kawe, Raiya Nassoro, amesema Kampuni ya CCCC wanashirikiana nayo imewasaidia katika Shule ya Msingi Kawe A na B ambapo walipatiwa vifaa zikiwemo mashine za kufulia na viti mwendo, kompyuta pamoja na vyakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule hizo.
Raiya amesema kampuni hiyo pia imewasaidia kujenga kingo za mto ili kuzuia uharibifu na kuwapa magreda ya kusafishia barabara ambapo wananchi na wadau mbalimbali wamekuwa wakichangia mafuta.
"Hii kampuni imeweza kuikumbuka ofisi yetu ya Serikali ya mtaa tumejumuika pamoja kwenye sherehe hii, kwa sababu ofisi zetu zinasahulika mara nyingi wanakumbukwa wabunge na madiwani hivyo, nawaomba wadau wengine wanaoishi kwenye mtaa wangu wakumbuke kushirikiana na jamii yetu," amesema Raiya.