DAR WAJIVUNIA ONGEZEKO LA WANAFUNZI, UFAULU ELIMU JUMUISHI
Augustino Ilomo (aliyekaa kwenye kiti mwendo) akipongezwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja (kulia), kutokana na kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Sita wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya utoaji elimu jumuishi nchini. Kushoto ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Deo Joseph.
Wakati Serikali ikiadhimisha miaka 30 ya utoaji wa elimu maalumu (jumuishi) nchini, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesema inajivunia ongezeko la udahili na ufaulu wa wanafunzi wenye ulemavu katika elimu ya awali, msingi na sekondari.
Miongoni mwa wanafunzi walioweka rekodi ya kufanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Sita ni Augustino Ilomo mwenye ulemavu wa viungo ambaye pia ni kiziwi kutoka Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa aliyepata daraja la pili Tahasusi ya Fizikia, Jografia na Hisabati (PGM).
Ilomo na wengine wanafanya ufaulu wa sekondari kwa wanafunzi wenye ulemavu katika halmashauri hiyo kuongezeka kutoka asilimia 50 mwaka 2022 hadi 82.5 mwaka 2024 huku udahili ukiongezeka kutoka asilimia 75 hadi 100.

Na Nora Damian, The Page

Kwa upande wa Elimu ya Awali na Msingi ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 90 mwaka 2022 hadi 100 mwaka 2023 huku wanafunzi walioandikishwa wakiongezeka kutoka asilimia 75 hadi 95.
Takwimu hizo zimetolewa Septemba 18,2024 na Ofisa Elimu Maalumu - Sekondari wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Pilly Ngalambe, wakati wa maadhimisho ya miaka 30 ya utoaji elimu jumuishi nchini ambayo katika ngazi ya halmashauri.
“Tunashukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu, tunaiomba Serikali iendelee kutoa vifaa saidizi pamoja na kuwezesha mafunzo kazini kwa walimu wataalam na wenye ulemavu ili kurahisisha utoaji wa elimu jumuishi kwa wanafunzi wote,” amesema Mwalimu Ngalambe.

Amesema manufaa mengine ni uboreshwaji wa miundombinu shuleni yaani ujenzi wa madarasa, matundu ya vyoo yaliyo rafiki kwa wanafunzi wenye ulemavu, chumba maalumu cha mtoto wa kike cha kujisitiri, ngazi mtelezo pamoja na lifti kwa majengo ya ghorofa.
Ofisa Elimu huyo amesema pia Serikali imenunua vifaa saidizi na vifaa vya kufundishia na kujifunzia, kuzindua kamusi ya lugha ya alama, kuboresha vyuo vya watu wenye ulemavu na ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi hao.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Deo Joseph, amesema wana wanafunzi 145 wenye ulemavu kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na wengi wanafanya vizuri kwenye masomo yao.
“Watoto hawapati sifuri tena kwa sababu wanasaidiwa na wenzao, anapoingia darasani anafundishwa wa pembeni yake anakuwa ni rafiki yake anamuwelewesha kinachofundishwa. Wanapokaa kwenye majadiliano wanasaidiana wote…kwa miaka miwili watoto wawili shuleni kwetu walifaulu kwa kupata ‘division one ya single digit’ wakaenda shule za vipaji, mmoja alikwenda Kibaha na mwingine Iliboru,” amesema Mwalimu Deo.
Diwani wa Viti Maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chamata, Beatrice Edward, amesema juhudi za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi kama vile kujenga miundombinu, kuwapa vifaa saidizi, kuwapeleka walimu kwenye mafunzo na nyingine zimeleta manufaa makubwa katika elimu jumuishi.

“Zamani tulizoea tunawatenga lakini sasa kupitia utekelezaji wa sera ya elimu jumuishi imewaweka pamoja, tunaona namna wanavyofanya vizuri kama watoto wasio na ulemavu, tunamshukuru Rais Samia kwa kuweka miundombinu rafiki inayowezesha watoto wenye ulemavu kusoma vizuri,” amesema Diwani Beatrice.
Diwani huyo amekuwa akifanya jitihada mbalimbali kusaidia watoto wenye ulemavu hasa kwa kuwapa vifaa saidizi kama vile fimbo kwa wasioona, mafuta na kofia kwa watoto wenye ualbino, viti mwendo na vingine.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye amewakilishwa na Flora Mgonja, aliwataka waliopewa dhamana kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kusimamia elimu jumuishi kwa kufanya kazi kwa umakini, weledi na ubunifu mkubwa.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo ‘Elimu jumuishi inayozingatia maadili, ujuzi, ubunifu na teknolojia kuleta usawa wa maendeleo kwa wote’ yalienda sambamba na tamasha ambapo wanafunzi wenye ulemavu wameonyesha vipaji vyao katika mchezo wa soka la mikono, golball, nyimbo, kukimbiza kuku na sanaa za maonesho na waliofanya vizuri walizawadiwa.