TAMASHA LA WANYAKYUSA KUFANYIKA DAR SEPTEMBA
Na Mwandishi Wetu, The Page
Umoja wa Kabila la Wanyakyusa kutoka sehemu mbalimbali nchini umeandaa tamasha linalotarajiwa kufanyika Septemba 27 hadi 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mgemi rasmi atakuwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.
Tamasha hilo litagharimu Sh milioni 250 na hadi sasa tayari Sh milioni 100 zimekusanywa huku wito ukitolewa kwa Wanyakyusa kumalizia kiasi kilichobaki.
Lengo la tamasha hilo ni kudumisha mila na desturi za Kabila la Wanyakyusa ambazo kwa sasa zinaonekana kupotea hasa kwa kizazi kipya.
Akizungumza Agosti 11,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za tamasha hilo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge, amesema umoja huo utasaidia kurudisha heshima ya Mbeya ambayo kwa sasa inaonekana kupotea.
Viongozi kutoka mkoani Mbeya wakiongoza harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya tamasha la Wanyakyusa.Umoja wa Kabila la Wanyakyusa kutoka sehemu mbalimbali nchini umeandaa tamasha linalotarajiwa kufanyika Septemba 27 hadi 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo mgemi rasmi atakuwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.
Tamasha hilo litagharimu Sh milioni 250 na hadi sasa tayari Sh milioni 100 zimekusanywa huku wito ukitolewa kwa Wanyakyusa kumalizia kiasi kilichobaki.
Lengo la tamasha hilo ni kudumisha mila na desturi za Kabila la Wanyakyusa ambazo kwa sasa zinaonekana kupotea hasa kwa kizazi kipya.
Akizungumza Agosti 11,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za tamasha hilo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Patrick Mwalunenge, amesema umoja huo utasaidia kurudisha heshima ya Mbeya ambayo kwa sasa inaonekana kupotea.
“Tamamduni za Kinyakyusa kwa sasa zimepotea, mfano kusalimiana kwa kuinama chini siku hizi hazipo kabisa, sasa kupitia tamasha hili ni wakati wa kuwakumbusha Wanyakyusa na kurudisha heshima yetu,” amesema Mwalunenge.
Mwakilishi wa Baraza la Wazee katika Mkoa wa Mbeya, Elius Mwakalinga, amewaomba Wanyakyusa kujitokeza kwa wingi kuchangia tamasha hilo ambalo litasaidia kudumisha tamaduni zao.
“Vijana wetu kwa sasa hawajui utamaduni wa makabila yao, tamasha hili litasaidia kurudisha maadili yetu ya Kinyakyusa kwa sababu hata kuongezeka kwa matukio mabaya ni vijana wetu kutokujua utamaduni wao," amesema Mwakalinga.
Tamasha hilo litaambatana na matukio tofauti kama vile kuzindua nyumba za asili za Kinyakyusa zilizojengwa katika Kijiji cha Makumbusho, maonesho mbalimbali ya tamaduni za Kinyakyusa ikiwemo ngoma ambapo zitapigwa ngoma zote za Kinyakyusa.
Ngoma hizo ni pamoja na Mang’oma ngoma amnayo huchezwa na watu wote, Magosi inayochezwa na vijana pamoja na ngoma ya Samba au Mababatoni ambayo wazee hupenda kucheza.
Ngoma nyingine ni ya Kitombwike pamoja na mchezo wa kupiga Mang’olong’ondo, pia kutakuwa na mavazi ya asili, vyakula vya asili, vifaa vya jadi, ufinyanzi, ususi wa mikeka, dawa na tiba za asili.
Mara ya mwisho tamasha la Umoja wa Kinyakyusa ulifanya tamasha mwaka 1996 ambapo la mwaka huu linatarajiwa kuwa la kipekee na watu takribani 3,000 wameonesha nia ya kushiriki.