SERIKALI YA MTAA MACHIMBO SEGEREA WAPEWA VITI
Na Heri Shaaban, Ilala
Kikundi cha Wanawake wa Mtaa wa Machimbo Kata ya Segerea wamemzawadia viti Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Mariam Machicha ili vitumike katika shughuli za kijamii na mikutano.
Machicha amepokea viti hivyo Agosti 15,2024 na kuwashukuru wanawake wa mtaa huo kwa ushirikiano wao.
"Nawapongeza wanawake wa Machimbo kwa umoja wao na kuisaidia Serikali yao ya mtaa, ofisi itawapa ushirikiano ili waweze kujikwamua kiuchumi na kusonga mbele katika kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," amesema Machicha.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wa Mtaa wa Machimbo, Emmy Mgota, ameishukuru Serikali ya Mtaa huo kwa utendaji bora na kuwapa ushirikiano kufikia mafanikio na malengo ya kukuza biashara.
Amesema kikundi hicho chenye malengo ya kujikwamua kiuchumi kwa kusaidia jamii inayowazuunguka kinashughulika kukodisha viti katika mikutano, misiba na sherehe mbalimbali kwa kuchangia fedha kidogo.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Machimbo, Isdory Sumuni, amekishukuru kikundi hicho na kuvitaka vikundi vingine kuiga mfano wa wanawake hao walioamua kuisaidia Serikali yao ya mtaa.