MBAGALA RANGITATU WABUNI MBINU KUPATA MAKUNDI ADIMU YA DAMU
Mwandishi Wetu, The Page
Hospitali ya Mbagala Rangitatu imeanzisha utaratibu wa kuwaunganisha pamoja kupitia kundi la WhatsApp watu wenye makundi adimu ya damu kukabili changamoto ya uhitaji huo.
Hospitali hiyo inatumia chupa za damu kati ya 150 mpaka 160 kila mwezi kuwahudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo akina mama wajawazito na watoto huku changamoto ikiwa katika kupata makundi adimu ya damu yenye vinasaba negative yaani hasi kama A, B, AB na O.
Akizungumza Agosti 9,2024 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangitatu, Dk. Ngalleny Amri, amesema kutokana na uhaba wa makundi adimu ya damu wataalamu wa maabara wameanzisha kundi la WhatsApp ambalo linawaunganisha watu wenye makundi adimu ya damu na ikitokea mtu anapata changamoto wanapigiwa simu ili wamchangie.
Dk. Amri alikuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya Taasisi ya Antul Akhlaaqual Islam (Jai) yaliyoenda sambamba na kuchangia damu salama kwa ajili ya hospitali hiyo.
"Tuna mahitaji makubwa ya damu katika kuokoa maisha ya wagonjwa wanaoletwa na inapotokea mgonjwa mwenye uhitaji lazima achangiwe na mwenye damu inayofanana na ya kwakwe.
"Katika hospitali yetu tunatumia chupa za damu kwa wagonjwa mbalimbali kuanzia 150 mpaka 160 kila mwezi ukiachilia mbali baadhi ya damu tunasafirisha katika vituo vingine vya kutolea huduma pale inapotokea kuna changamoto," amesema Dk. Amri.
Ameipongeza taasisi ya Jai kwa ubunifu wao na kuwaomba wadau wengine waige mfano huo kuokoa maisha ya Watanzania wenye uhitaji.

Amesema wananchi waendelee kujitokeza kuchangia damu kwani hakuna kiwanda cha kutengeneza damu na wala haiuzwi hivyo lazima damu itoke kwa binadamu mwingine.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Jai Mbagala Zakhem, Amini Kiungulio, amesema kilele cha maadhimisho ya taasisi ya Jai ni Agosti 13,2024 ambayo yatafanyika jijini Mwanza na wamekubaliana kila kituo cha taasisi hiyo kiwe na siku maalumu ya kuchangia damu kwa hiari kwa lengo la kuisaidia jamii.
"Katika maadhimisho yetu tumekubaliana tukusanye chupa za damu 300 katika kituo chetu cha Mbagala Zakhem hivyo, tunaiomba jamii ichangie damu ili kuokoa akina mama wajawazito, watoto wadogo na wahanga mbalimbali," amesema Kiungulio.
Mmoja wa wachangiaji damu, Issa Kindi, amesema ametoa damu ili kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji na kuokoa maisha yao.