WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU KAWE WAOMBA KUKARABATIWA MADARASA

Mwandishi Wetu, The Page


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kawe, Cathbert Mfwangaro amesema
wamelazimika kuwahamisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu baada ya mapaa ya madarasa yao kuvuja huku kuta zikiwa na nyufa.

Hayo yamesemwa wakati akipokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu uhitaji kutoka Kampuni ya Ujenzi inayomilikiwa na Serikali ya China (CCCC) Tawi la Tanzania pamoja na kupatiwa matibabu bure na madaktari kutoka China.

Mfwangaro amesema wanafunzi hao wakiwemo wenye usonji wana madarasa matatu ambayo wameyatumia kwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati hivyo yana nyufa na paa zinavuja na kulazimika hatua iliyosababisha kuwahamisha kwenye madarasa mengine.
"Wahandisi wa Manispaa ya Kinondoni walipita mwaka 2023 walitushauri tusiwaweke wanafunzi kwenye madarasa ambayo paa zinavuja hadi yatakapokarabatiwa," amesema.

Amesema wamewahamisha wanafunzi hao na kuwapeleka katika madarasa mengine Ili wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye usonji wapate nafasi.

Pia ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa msaada kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu shuleni hapo wakiwemo wa usonji, wenye ulemavu wa viungo, wasioona na kwamba wote wanawalea sawa na wanafunzi wengine kwa kuwapa kipaumbele katika changamoto zao ili waweze kujifunza zaidi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kawe, Husna Nondo, ameishukuru kampuni ya CCCC kwa kutoa vifaa tiba, viti mwendo, friji, mashine ya kufulia na vyakula kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalumu.

Naye Kiongozi wa Timu ya Madaktari kutoka China, Zhang Kai, amesema wapo madaktari zaidi ya kumi wanaotibu magonjwa mbalimbali ikiwemo moyo na binadamu.

"Pia tunatoa huduma ikiwemo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na shuleni na kwa wanafunzi hawa tumejitolea kuwahudumia na kuwapima bure," amesema Kai.
Powered by Blogger.