PURA KUTAFUTA WAWEKEZAJI WAPYA WA GESI, MAFUTA
Mwenyeiti wa Bodi ya PURA, Halfani Halfani, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea banda la mamlaka hiyo kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, Dar es Salaam.
Akizungumza Julai 11,2024 kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, Halfani Halfani, amesema kwa muda mrefu kumekuwa hakuna wawekezaji wa kutosha na kwamba maeneo mengine ambayo yalikuwa na wawekezaji yamerudishwa serikalini.
“Miradi tunayoifanyia kazi kwa sasa na ambayo ni kipaumbele cha serikali ni kuhakikisha kwamba tunatafuta wawekezaji, tuna jukumu la kutafuta wawekezaji kwenye maeneo ambayo yako wazi. Taasisi imekuwa inafanya matayarisho ya mikutano ya kutangaza maeneo ili wawekezaji waje…tunatarajia katika robo ya kwanza ya mwaka ujao huenda ikafanyika,” amesema Halfani.
Amesema mpaka sasa yapo maeneo yanayozalisha gesi kama vike Songosongo wilayani Kilwa, Mazi Bay Wilaya ya Mtwara Vijijini lakini mwaka huu serikali imetoa leseni ya uendelezaji kwa mwekezaji aliyeko Wilaya ya Mtwara (eneo la Ntoria) ambapo wanatarajia ataanza uzalishaji wa gesi mwakani.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mwekezaji huyo atakuwa na uwezo wa kuzalisha futi za ujazo milioni 100 kwa siku kiwango ambacho kitaongezeka kadiri soko linavyozidi kuimarika na uwezo wa visima kuzalisha.
“Mwekezaji atakapoanza kuzalisha tutakuwa na uhakika kwamba tutaendelea kupata gesi kwa mitambo tuliyoiweka hapa nchini kwa muda mrefu, tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba hatutakuwa na uhaba wa gesi kwa kutafuta wawekezaji wapya na kuhakikisha waliopo wanazalisha kwa ufanisi,” amesema.
PURA ina jukumu la kumshauri Waziri wa Nishati masuala ya mkondo wa juu wa petroli yaani utafutaji, uzalishaji na usambazaji wa gesi nchini, kusimamia ufanisi wa sekta ya utafutaji na uzalishaji na kuhakikisha Watanzania wanashiriki kwenye shughuli za utafutaji na uzalishaji.
Majukumu mengine ni kusimamia shughuli za uuzwaji wa gesi nje ya nchi, kutunga sheria ndogo za kuhakikisha sekta hiyo inafanya kwa ufanisi na usalama.
Na Nora Damian, The Page
Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli na Gesi Asilia (PURA) imesema imejipanga kuongeza wawekezaji katika utafutaji wa gesi na petroli nchini kwa kuwa ndicho kipaumbele cha serikali.