NAIBU WAZIRI AJIUZULU, ATAJA SABABU

Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Na Mwandishi Wetu, The Page

Mbunge wa kuteuliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amejiuzulu wadhifa huo.

Mbarouk ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge, amemuandikia Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson barua ya kujiuzulu ubunge leo Julai 21,2024.

Kulingana na barua hiyo, Mbarouk amesema amefikia uamuzi huo kutokana na changamoto za kijamii zinazomkabili kwa sasa.

“Ninalazimika kuchukua uamuzi huu wa kujiuzulu ili nipate nafasi ya kushughulikia changamoto hizo,” amesema Balozi Mbarouk.



 


Powered by Blogger.