RAIS SAMIA: USALAMA WA MTOTO NI JUKUMU LA JAMII NZIMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.


Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu.

