DK. TULIA, MKURUGENZI MKUU NSSF WATETA KUHUSU ULIPAJI MAFAO
Na Mwandishi Wetu, The Page
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba kuhusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao umeboresha kupitia mifumo ya Tehama.
Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 28,2024
baada ya kuhitimisha Bunge jijini Dodoma.
Mshomba pia ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kujali masilahi ya Watanzania.
Mkurugenzi huyo pia amempongeza Dk. Tulia kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.

