MAKAMBA AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI NORDIC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba (Katikati), akiongoza Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Nordic na Afrika kinachofanyika Copenhagen Denmark.
Na Mwandishi Maalumu, Copenhagen Denmark
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba ameongoza sehemu ya kwanza ya Kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Nordic na Afrika ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya kikao hicho.
Mawaziri hao waliokutana jijini Copenhagen nchini Denmark wametoa hoja mbalimbali za kukuza ushirikiano kati ya nchi za Afrika na za Nodric pamoja na kuimarisha mwelekeo wa vikao vijavyo vya Nordic ikiwa ni pamoja na kuwa na viongozi wa muda.

Kutokana na kuwa masuala mengi yanayojadiliwa kuwa ni ya kiuchumi na uwekezaji, imependekezwa kuwa pengine upo umuhimu wa kuanzishwa kwa Mkutano wa Mawaziri wa sekta hizo wa Nchi za Afrika na Nordic ili kurahisisha utekelezwaji wa yale yanayoafikiwa.
Msisitizo mkubwa katika mkutano huu umehimiza kuwepo kwa sauti ya pamoja katika masuala ya kimataifa, kutumia vyema nguvu - kazi vijana katika mipango ya mbeleni, kuhamasisha na kulinda amani duniani kote.