WAZIRI UMMY: MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA NAMBA ZINAONGEA
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miaka mitatu ya Rais Samia na mageuzi katika sekta ya afya nchini.
Zaidi ya Sh trilioni 6.722 zimetumika katika sekta ya afya kutekeleza vipaumbele mbalimbali na kuimarisha huduma za afya nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Hatua hiyo imewezesha kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 8,549 mwaka 2021 hadi kufikia 9,610 Machi 2024 sawa na ongezeko la vituo 1,061.
Hayo yamesemwa leo Machi 18,2024 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu miaka mitatu ya Rais Samia na mageuzi katika sekta ya afya nchini.
“Ongezeko la vituo vya kutoa huduma za afya nchini na maboresho ya miundombinu yaliyofanyika yametuwezesha kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi kama tunavyoelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025. Wananchi wanapata huduma za afya ndani ya kilomita tano ya maeneo yao wanayoishi,” amesema Ummy.
Amesema kati ya fedha hizo Sh trilioni 1.02 zimetumika kujenga na kufanya maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo mapya, ukarabati na kukamilisha ujenzi wa hospitali mpya katika mikoa mipya mitano.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy, wamekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini Mtwara na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato na tayari zimeanza kutoa huduma.
Eneo lingine ni ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Katavi, Njombe, Songwe, Simiyu na Geita na kuhamisha hospitali nne kutoka majengo yake ya zamani kwa kujenga mpya ambazo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Singida, Mara na Ruvuma.
Vilevile kukarabati majengo mapya ya kutolea huduma za afya katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Ligula (Mtwara), Sekoutoure (Mwanza), Maweni (Kigoma), Sumbawanga (Rukwa) na Kitete (Tabora).
Pia ujenzi wa mitambo 21 ya kuzalisha hewa tiba ya oksijeni kwa ajili ya wagonjwa mahututi na wagonjwa wa dharura.
Na Nora Damian, The Page

Amesema pia wamenunua vifaa tiba vya uchunguzi na matibabu ya wagonjwa vyenye thamani ya Sh bilioni 290.9 ambavyo vinapatikana kuanzia ngazi ya hospitali ya taifa hadi hospitali za rufaa za mikoa na halmashauri.
“Kipimo cha CT Scan sasa kinapatikana katika hospitali 27 kati ya 28 za rufaa za mikoa nchini, kwa mwaka 2023 jumla ya wagonjwa 15,386 walipatiwa huduma za kipimo cha CT Scan,” amesema.
Kuhusu vitanda vya kulaza wagonjwa amesema viomeongezeka kutoka 86,131 mwaka 2021 hadi kufikia 126,209 Machi 2024.
Waziri huyo amesema pia Serikali imekamilisha ujenzi wa wodi 45 za wagonjwa mahututi katika hospitali ngazi ya taifa, maalumu, kanda na mikoa na kuziwekea vifaa tiba hatua iliyoongeza idadi ya vitanda kutoka 258 mwaka 2021 hadi 1,362 mwaka 2023.
Amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa ICU 28 katika ngazi ya halmashauri ambapo 27 kati ya hizo zimekamilika na moja iko hatua ya ukamilishaji.
Kuhusu dawa amesema katika kipindi hicho Sh bilioni 20 zimekuwa zikitolewa kila mwezi hatua iliyowezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawa muhimu na bidhaa nyingine za afya aina 290.
Kwa upande wa afya ya uzazi, mama na mtoto amesema wamekamilisha ujenzi wa jengo la kutoa huduma za afya ya mama na mtoto Meta lililopo katika Jiji la Mbeya lililogharimu Sh bilioni 13.2.
“Tunaendelea na majengo ya huduma za mama na mtoto kwenye hospitali za rufaa za mikoa ambazo ni sekoutoure, Geita, Simiyu, Mawenzi, Njombe na Songwe ambazo zimegharimu Sh bilioni 71.1,” amesema Waziri Ummy.
Amesema Serikali imeimarisha huduma za upasuaji wa wajawazito kwa kuongeza vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni kutoka 340 mwaka 2021 hadi kufikia 523 mwaka 2023.
Aidha amesema wameanzisha wodi maalumu za huduma za watoto wachanga wagonjwa ambapo hadi kufikia Desemba 2023 hospitali 189 zinatoa huduma hiyo ikilinganishwa na hospitali 165 mwaka 20222 na hospitali 14 mwaka 2018.
Waziri Ummy amesema mashine 140 za uchunguzi wa saratani zimenunuliwa na kusambazwa kwenye vituo 140 vya kutolea huduma za afya katika halmashauri 104 katika mikoa 26 ambavyo vina thamani ya Sh bilioni 1.1.
Waziri Ummy amemshukuru Rais Samia kwa maono yake na kuwezesha kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za afya na kuwapongeza watumishi kwa kazi ya kuhudumia wananchi.